Home Kitaifa TBS WATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI , WAFANYA BIASHARA NA WADAU SABASABA

TBS WATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI , WAFANYA BIASHARA NA WADAU SABASABA


Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakiendelea kuwahudumia wananchi waliotembela banda la TBS katika Maonesho ya ya  48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja Vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam

W

Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Francis Mapunda akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya ya  48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja Vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa huduma kwa wajasiriamali ,wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Viwango katika Maonesho ya  48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba ambapo wamekuwa wakiwapa taarifa ya huduma ambazo wanazitoa ikiwemo uandaaji wa viwango,usajili wa bidhaa na majengo ya vyakula na vipodozi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Julai 9, 2024 kwenye maonesho hayo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Francis Mapunda amesema wameweza kupata wadau mbalimbali wakiwemo wajasirimali wadogo ambao wameweza kupata elimu namna ya bidhaa zao zinavyotakiwa kuthibitishwa ubora na Shirika hilo kupitia SIDO.

“Katika maonyesho haya pia tunatoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaeleza kuhusu huduma tunazozitoa ikiwemo kuthibitisha ubora wa bidhaa, mifumo ya kimenejimenti, upimaji, kufanya usajili wa vyakula na vipodozi” amesema 

Aidha amesema kupitia Maonesho hayo wanapokea wajasiriamali wadogo waliosajiliwa na kutambulishwa kwao na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ambao wanawapatia huduma ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bila malipo.

Amesema baada ya kwenda SIDO watafanyiwa tathimini na kuandikiwa barua ya utambulisho kwenda TBS ambako watahudumiwa bure kwa miaka sita wakati wakiwa wanaendelea kukuwa kibiashara. 

Pamoja na hayo Mapunda ametoa wito kwa wafanyabiashara na walaji kuhakikisha kwamba bidhaa wanazozinunua ziwe zimethibitishwa na kuwa na alama ya ubora ya TBS, na wanaofanya biashara ya chakula na vipodozi wasajili majengo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!