Home Kitaifa TBS WATANGAZA KUFANYA MAKUBWA KWA WATEJA WAO SABASABA

TBS WATANGAZA KUFANYA MAKUBWA KWA WATEJA WAO SABASABA

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewakaribisha wafanyabiashara, wenye viwanda pamoja na wananchi kwa ujumla kutembelea banda lao katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 03,2022 katika Maonesho hayo Afisa Uhusiano TBS, Bi.Neema Mtemvu amesema Maonesho hayo yamewawezesha kuwakutanisha na wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kupata huduma mbalimbali kwenye banda lao na kuweza kutatua changamoto ambazo wanakutana nazo wafanyabiashara.

“Kuna wale ambao wanahitaji kufahamu masuala ya Viwango, wanafika hapa tunamuelezea ni namna gani ambavyo ana umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa kuandaa viwango na vilevile kama anataka kiwango ni namna gani anakipata na hapahapa tunaweza kumuwezesha pia akipate”. Amesema

Amesema huduma zote ambazo zimekuwa zikitolewa makao makuu ya TBS au katika ofisi zao za Kanda unaweza ukizipata ukitembelea banda lao katika maonesho hayo ambayo yanayoendelea kwenye viwanja hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!