Home Kitaifa TBS WASHIRIKI MAONESHO YA 21 YA WAHANDISI TANZANIA KWA KISHINDO

TBS WASHIRIKI MAONESHO YA 21 YA WAHANDISI TANZANIA KWA KISHINDO

 SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Maonesho ya 21 ya Wahandisi Tanzania  kwa kutoa elimu kwa wahandisi kuhusu uwepo mashine bora na za kisasa katika maabara ya TBS ambazo wanaweza katika miradi yao kuhakiki bidhaa katika miradi yao.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) Dkt. Ashura Katunzi katika Banda la TBS 
 Maonesho ya 21 ya Wahandisi Tanzania Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 6, 2024 katika Maonesho hayo ambayo yamefanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wahandisi TBS, Mhandisi Mohammed Kaila amesema TBS limefanya uwekazaji mkubwa katika swala la mashine za  kupima ubora wa bidhaa.

Amesema uwekezaji uliofanywa na  TBS kwenye suala la mashine, kuna Hydrostatic Test Pessure Machine ambazo zinaweza kupima mabomba kuanzia kipenyo cha milimita 12 mpaka ya milimita 800 na mashine hiyo ni miongoni kwa mashine 5 tu zinazopatikana Afrika.

Aidha amesema miongoni mwa mashine zilizopo TBS pia kuna mashine nyingine ya kupima Solar katika mazingira yoyote bila kuzingatia uwepo wa jua tu na ni mashine pekee inayoweza kufanya hivyo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kato.

Pamoja na hayo Mhandisi Kaila amewataka wahandisi pamoja na wakandarasi kutembelea banda la Shirika hilo katika maonesho hayo ili waweze kupata elimu ya viwango na kuweza kutoa huduma zenye viwango na bora katika miradi yao kwa jumla. 

Ameeleza namna walivyojipanga katika kutoa elimu mbalimbali huku akiwataka wahandisi wote watumie Viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!