Home Kitaifa TBS: WANANCHI MSINUNUE BIDHAA ZISIZO NA VIWANGO

TBS: WANANCHI MSINUNUE BIDHAA ZISIZO NA VIWANGO

Na Boniface Gideon-TANGA

Shirika la Viwango Nchini (TBS) limewataka Wananchi kuacha kutumia bidhaa zisizokuwa na alama ya Shirika hilo ili kuepusha madhara Makubwa yanayoweza kutokea kwa mtumiaji ikiwemo madhara ya kiafya kwa bidhaa za vyakula, vipodozi na hasara ya kupoteza pesa kwa bidhaa zisizo za vyakula kama vile Ujenzi.

Akizungumza na Waandishi wa mapema leo wakati wa zoezi la kutoa Elimu kwa Wadau mbalimbali wanaotembelea banda la ‘TBS’ kwenye maonyesho ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga,
Meneja Mahusiano na Masoko, Gladness Kaseka amesema bidhaa zisizokuwa na alama ya ‘TBS’ zinakuwa hazijahakikiwa hivyo ni hatari kwa watumiaji.

“Bidhaa zote za ndani na nje ya Nchi zinatakiwa ziwe na ubora,na ili ujue ubora ni lazima uone alama ( Nembo yetu ) kwenye bidhaa husika, madhara yapo mengi na yanayokana na aina ya bidhaa husika kulingana na matumizi yake mfano bidhaa za Ujenzi, unaweza ukanunua mabati yasiyokuwa na ubora na baada ya muda utakuta yanavuja na ukinunua bidhaa kama za vyakula na vipodozi hizi zote ni bidhaa zinazoleta athari za Kiafya endapo mtu atatumia bidhaa isiyokuwa na Viwango” amesisitiza Gladness

Gladness amewataka Wafanyabiashara na Wazalishaji wa Bidhaa kuzingatia sheria na kanuni kwakuhakikisha bidhaa wanazozalisha au kuuza zinakuwa zimekidhi vigezo vya Ubora kutoka Mamlaka hiyo.

“Wito wetu kwa Wafanyabiashara na Wazalishaji wa Bidhaa, hakikisheni mnafuata Sheria na taratibu kwa mujibu wa Sheria ukikutwa na bidhaa isiyokuwa na Viwango unapigwa faini kuanzia Sh.10Mil. na isiyozidi mil.100, sisi tupo kwaajili ya kuwahudumia wakati wowote” amesema Gladness

Kwa upande wake Mwanamkuu Hassan mtumiaji wa bidhaa za vipodozi, aliishukuru ‘TBS’ kwa Elimu hiyo nakwamba awali alikuwa hana uelewa juu ya vipodozi,

“Kiukweli mimi hapo awali sikuwa na uelewa juu ya vipodozi ninavyovitumia kama vinatakiwa viwe na alama ya ‘TBS’ nimeshaunguzwa sana na vipodozi na nimetumia gharama kubwa kujitibu, niliungua usoni nilikuwa na mabakamabaka na miguu ilibabuka na kuweka alama nyeusi” amesema Mwanamkuu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!