Home Kitaifa TASAC YAFANYA SENSA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI NA SADC YA VYOMBO VIDOGO...

TASAC YAFANYA SENSA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI NA SADC YA VYOMBO VIDOGO VYA MAJINI

Dar es salaam,

Na Emmanuel Kawau.

Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) lazindua ripoti ya sensa ya vyombo vidogo vya usafiri majini ambayo ni ya kwanza kuwahi kufanyika katika nchini za Afrika Mashariki na ukanda wa SADC kwa ujumla.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo Jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia sekta ya Uchukuzi Antupele Mwakibete amesema ripoti hiyo itasaidia kuboresha sera,kubainisha fursa zilizopo katika kukuza uchumi wa Taifa na watu wake kupitia uchumi wa Bluu.

Pia amewataka wadau mbalimbali kutumia taarifa hiyo kibiashara kwa kuangazia maeneo yenye vyombo vingi kufungua biashara za uuzaji wa vipuri vya boti,maboya,injini na vifaa vingine.

Kwa mujibu wa taarifa ya sensa jumla ya idadi ya vyombo vidogo vya majini ni 52,189,pia kuna jumla ya mialo 885,idadi ya vyombo vidogo vya majini vyenye urefu wa mita nne au zaidi kwenye maeneo ya maji ni 45,976,kati ya hivyo Asilimia 53.65% vipo Ziwa Victoria, 13.41% vipo Bahari ya Hindi,10.28% vipo Ziwa Tanganyika,7.65 vipo Ziwa Nyasa na Asilimia 15.1% vipo katika maeneo mengine ya maziwa na mabwawa nchini” Amesema Antupele.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkeyenge amesema katika uandaaji wa sensa hiyo wameshirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),Wizara ya ujenzi na uchukuzi,Tamisemi, Wizara ya mifugo na uvuvi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya Uchukuzi.

Ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa sensa hiyo wameweza kuunda kanzi data maalumu inayorahisisha kuvitambua vyombo,wamiliki na maeneo vilipo na kurahisisha utambuzi wa vyombo na hali yake na endapo kikitapata majanga kuweza kukifikia kwa haraka na kutambua ni chombo kipi kimehusika kwenye ajali au changamoto yoyote majini.

Nao Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema ni mara ya kwanza NDS imeshiriki katika sensa ya vyombo vya majini hivyo wamewapongeza TASAC kwa hatua hiyo na kuongeza kuwa kanzi Data iliyoundwa itasaidia sana Wafanyabiashara,wadadisi na watafiti mbalimbali kufanyakazi yao kwa urahisi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!