Home Michezo TARURA YAENDELEZA UBABE KWA KUIPIGA ARDHI 1-0

TARURA YAENDELEZA UBABE KWA KUIPIGA ARDHI 1-0

Timu ya Mpira wa miguu ya TARURA yaendeleza ubabe kwa siku tatu mfululizo ambapo Leo imefanikiwa kuipiga Ardhi goli 1-0 kwenye mashindano ya SHIMIWI.

Katika mchezo wa Leo uliochezwa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Mkwawa,TARURA ilifanikiwa kuona goli la ardhi katika kipindi cha kwanza dakika ya 28 ambapo mchezaji Erick Tegamaisho aliipatia goli la ushindi.

Hadi mwisho wa mchezo huo timu ya Ardhi haikufanikiwa kuliona goli la TARURA licha la mchezaji wa TARURA Makunge Mwera kupewa kadi nyekundu.

Hadi Leo TARURA inaongoza kwa kuwa na point 9 na magoli 8 ambapo katika mechi ya kwanza dhidi ya Wakili Mkuu iliibuka kidedea kwa magoli 4-0 na katika mechi ya pili dhidi ya Wizara ya Elimu ilitoka mshindi kwa 3-2.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!