Home Kitaifa TARURA PANGANI YAMALIZA CHANGAMOTO YA KUJAA MAJI MAKAZI WAKATI WA MVUA.

TARURA PANGANI YAMALIZA CHANGAMOTO YA KUJAA MAJI MAKAZI WAKATI WA MVUA.

NA. BONIFACE GIDEON, PANGANI

Wakala wa barabara za vijijini (TARURA) Wilayani Pangani imesema katika kuhakikisha changamoto za miundombinu ya Barabara za Vijijini katika wilaya hiyo serikali imewekeza zaidi ya sh. Billion tatu inatoka katika maeneo matatu tofauti, ikiwa ni pamoja na fedha za tozo na mfuko wa barabara.

Hayo aliyasema Meneja wa Tarura Wilayani pangani Eliya Mgaya wakati akizungumza na waandishi wa habari Jana Wakati akifanya Ukaguzi wa Ujenzi wa Barabara zinazoendelea kujengwa na kufanyiwa Ukarabati ambapo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imejipanga kuhakikisha miundo mbinu ya barabra katika wilaya hiyo inakuwa rafiki kwa wananchi wake .

Alisema miongoni mwa changamoto kubwa ambayo imefanyiwa kazi ni pamoja kujenga mifereji ya kuondoa maji kwenye makazi ya watu kazi iliyofanyika kwa miaka mitatu mfululizo.

Aidha aliongeza kuwa miradi inayoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Mhunguli ambayo inagharimu kiasi cha sh.milion 750 na mradi wa ujenzi wa kiwango cha Lami nyepesi katika barabra za Pangani inayogharimu kiasi cha sh. Million 250 ambayo ni ya mita 900 ambapo mkandarasi anaendelea na kazi.

Sambamba na hayo alisema fedha za tozo imelekezwa katika miradi mitatu ambapo ni pamoja na barabara za changarawe katika barabara za wilaya ya Pangani ambapo kazi bado inaendelea .

Utekelezajia unaendelea wa miradi ya kuendeleza barabara kupitia fedha za mfuko wa barabara ambapo fedha za kawaida ni sh.bilioni 1.1 ambapo fedha za jimbo milioni 500 inajenga mita 900 na milioni 150 inajenga kiwango cha Lami nyepesi.” alisema Mgaya.

Meneja Mgaya alisema kuwa kutokana miundombiunu ya barabara hiyo alisema kuwa wametafutia njia mbadala ambayo urefu wa mita 800 ambayo imegharimu kiasi cha milioni milioni 70 ambayo imetumika kukata mlima na uwekaji wa kokoto kazi abayo bado inaendelea .

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa wilaya pangani katika kijiji cha mnyomgeni wamipongeza hatua hiyo ya serikali kuwasaidia kujenga mifereji kwa ajili ya kuondoa maji kwenye makazi yao .

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Mnyongeni Hassan Issa alisema kuwa changamoto ya maji kujaa kwenye zo ilidumu kwa muda mrefu hivyo ameishukuru serikali kuwaboreshea miundo mibinu hiyo ambayo hapo iliwasababishia hata kuhama nyumba zao kipindi cha mvua kwani maji yalikuwa yanafika mpaka kwenye viuno.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!