Home Kitaifa TARURA MWANZA YAHITAJI BILIONI 6.3 KURUDISHA MIUNDOMBINU KATIKA UBORA

TARURA MWANZA YAHITAJI BILIONI 6.3 KURUDISHA MIUNDOMBINU KATIKA UBORA

Na Neema Kandoro Mwanza

MENEJA wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Tanzania (TARURA) Mkoani Mwanza amesema mvua za Elnino zinazoendelea kunyesha zimesababisha uharibifu wa zaidi ya sh bilioni 6.3 kwa miundo mbinu yake.

Hayo yamebainishwa Leo jijini hapa na Meneja wa TARURA mkoani Mwanza, Mhandisi Makori Kisare akisema maeneo ambayo yameathiriwa zaidi ni wilaya ya Sengerema na Buchosa ambapo kiasi cha sh bilioni zinahitajika kurudisha miundo mbinu katika ubora wake.

Alisema maeneo mengine yaliyoathiriwa kuwa ni barabara ya wilaya ya Magu, Misungwi, Ilemela, Kwimba na Nyamagana ambapo kingo za daraja la Mwananchi zikiathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa.

“Madhara hayo yanatofautiana kati ya eneo moja na jingine huku maeneo ya Jijini Mwanza yakiwa hayajapata madhara zaidi kutokana na uwepo wa ardhi ya miamba” alisema Mhandisi Makori.

Mhandisi Makori alibainisha kuwa takwimu hiyo ni hadi kufikia tarehe 4 Disemba ambapo wanaendelea kuwasihi wananchi kutunza mazingira vizuri kuepueka uharibifu unaoweza kusababisha madhara kwa barabara nyakati hizi za mvua kubwa.

Aliwataka wananchi kuepuka kutupa taka hovyo ambazo zinaweza kuziba kwenye mitaro ya maji na hivyo kuleta madhara yanayoweza kusababisha maji kusambaa na kuathiri makazi ya watu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!