Home Kitaifa TARURA MANISPAA YA MUSOMA YAOMBA FEDHA ZA DHARURA KUREKEBISHA BARABARA

TARURA MANISPAA YA MUSOMA YAOMBA FEDHA ZA DHARURA KUREKEBISHA BARABARA

Na Shomari Binda-Musoma

OFISI ya Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) manispaa ya Musoma kupitia Tarura mkoa wa Mara umeomba kiasi cha shilingi milioni 239.950.600.00 kulekebisha barabara.

Maombi hayo yamekuja kufuatia mvua nyingi zilizonyesha kuanzia mwishoni mwa mwezi machi hadi mwanzoni mwa mwezi mei 2023.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za barabara robo ya tatu mwaka wa fedha 2022/2024, kwenye kikao cha baraza la madiwani,mhandisi wa Tarura manispaa ya Musoma Muhamed Etanga kwa niaba ya meneja mhandisi Joseph Mkwizu amesema tayari maombi yameshawasilishwa.

Amesema mvua hizo zimepelekea uharibifu mkubwa wa baadhi ya barabara na hatua za makusudi zomechukuliwa kwa kufanya marekebisho.

Etanga amesema licha ya kuwasilishwa kwa maombi hayo lakini hadi sasa hawajaidhinishiwa kiasi chochote cha fedha.

Amesema barabara ambazo zinahitaji matengenezo ya dharura kutokana na mvua hizo kuwa ni Songe, majengo mapya, Buhare, Mwisenge, Makoko, Bweri, Kwangwa, Mwisenge, Misango pamoja na Mshikamano.

Mwakilishi huyo wa meneja wa Tarura manispaa ya Musoma amesema miongoni mwa changamoto ni mvua za misimu miwili kwa mwaka ambazo zinapelekea uharibifu wa mara kwa mara.

Wakipokea taarifa hiyo,madiwani wa mamispaa ya Musoma wamepongeza kazi nzuri inayofamywa na Tarura kwenye Kata zao licha ya changamoto ndogo.

Wamesema kazi inayofanywa na Tarura manispaa ya Musoma zinaonekana na maeneo mengi ambayo yalikuwa hayapitiki na sasa yanapitika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!