NA MWANDISHI WETU
Tanzania imekuwa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika katika upande wa usafiri wa Anga (SASO) baada ya kutia saini mkataba wa kuridhia kuwa mwanachama.
Zoezi hilo limefanywa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ambapo mkataba huo utasimamia Usafiri wa anga kwa niaba ya Tanzania na hatua hiyo itapelekea kufunguka kwa fursa za kujifunza miongoni mwa nchi wanachama hususani kujua ya utendaji kwenye usafiri huo.