Home Kitaifa TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINE KUADHIMISHA MIAKA 78 YA UN

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINE KUADHIMISHA MIAKA 78 YA UN

Na Magrethy Katengu

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imesema itaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya uwekezaji kwa vijana kuhakikisha inainua ustawi wa wao wa kiuchumi kwa miaka ya sasa baadae

Hayo yamesemwa leo Oktoba 24, 2023 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba ( Mb) katika Maadhimisho ya miaka 78 ya Umoja wa Mataifa ambapo kwa Tanzania imefanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es na juongizwa na ”Kaulimbiu ya Siku ya Umoja wa Mataifa ni” Kuinua Idadi ya Vijana wa Tanzania

Waziri Kairuki amesema vijana idadi yao ni 60% hivyo serikali haina budi kutumia njia mbalimbali za kuwekeza mekuwa ili kuhakikisha wanafaidika kiuchumi sass na baadae waepukane.na kuwa tegemezi wakilalamika hakuna ajira .

Tanzania Bara, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 inafanyiwa mapitio ili kuakisi hali ya sasa ya maendeleo ya vijana, vipaumbele na changamoto” Mhe. Kairuki amesisitiza

Ametajae moja ya mkakati ni kuwezesha vijana kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo hutoa mikopo kwa vijana wajasiriamali na uanzishwaji wa zaidi ya mifuko 45 maalum katika wizara na idara mbalimbali ili kuhakikisha kuwa vijana wanawezeshwa kiuchumi.
Amefafanua kuwa Serikali ya Tanzania imehakikisha kuna ongezeko la upatikanaji wa huduma za ushauri nasaha rafiki kwa vijana kupitia programu ya Afya ya Ujinsia na Haki za Uzazi na kuongeza upatikanaji wa huduma za matunzo na matibabu ya VVU.

Amesema kupitia Mpango wa Kujenga Kesho Bora – YOUTH INITIATIVE FOR AGRIBUSINESS, Serikali inatarajia kuongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo na kuharakisha kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kwa ajili ya maisha endelevu na bora.

Kufuatia juhudi hizo, bado vijana wameendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali hivyo, Mhe. Kairuki amezitaka jumuiya zote za Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kikanda kuwa na nguvu ya pamoja ili kuweka sera na mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki amewaasa vijana kuwa wabunifu na kutumia teknolojia ambayo ni nguzo muhimu za kukuza uwezeshaji wa vijana.

Ni muhimu kusaidia wajasiriamali wachanga katika kubadilisha mawazo yao kuwa biashara zinazofaa, endelevu kupitia kujenga uwezo na upatikanaji wa masoko na matumizi ya teknolojia na uvumbuzi.” amesema.

Waziri Kairuki amesisitiza umuhimu wa amani umoja na mshikamano pia ameshukuru Umoja wa Mataifa kutokana na ushirikiano wao na Tanzania katika kusaidia kutekeleza mpango wa miaka mitano wa maendeleo hadi 2030.

Nae mkuu wa chuo Cha ulinzi na usalama Tanzania brigedia generali George mtang’are ambaye alimuwakilisha mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania Jacob Mkunda amesema Tanzania ni miongoni kwa Nchi mshiriki katika masuala ya uliznia wa amani ambapo Hadi Sasa anashika nafasi ya 12, ana vikosi vya ulinzi congo,Nchi ya afrika ya kati Lebanon,Jamuhuri ya Afrika ya kati

Hata hivyo amebainishakwamba wakati tunasherehekea miaka 78 ya umoja wa mataifa lakini kwa miaka mingi kumekuwa na changamoto ya masuala ya ulinzi na usalama katika baadhi ya Nchi ikiwemo congo,

Akifafanua kuhusu Nchi ya Congo amesema vikosu walivyovipeleka wamefanikiwa kwa kiasi kurejesha amani ambapo wamefanya kazi kubwa sana ya kupambana na vikosi vya M 23

Lazima tukubali kwamba amani inaanzia kwa wananchi wenyewe Mimi ninachosema kwamba umoja wa mataifa uko kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wawe na amani na utulivu” amesema Mtang’are.

.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!