Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Nchi , Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji (SMZ) Bw. Khamis Suleiman Mwalim
wakati akiongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) ngazi ya Makatibu Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi , Congo DRC na Sudani Kusini kilichofanyika jijini Arusha tarehe tarehe 30 Mei 2024.
Ujumbe wa Tanzania ulijumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TANTRADE), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Tume ya Ushindani (FCC) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Mamlaka ya kuhusu Uwekezaji Zanzibar (ZIPA)