Home Kitaifa TANZANIA YASAINI MAKUBALIANO MKUTANO WA ITU PP 2022

TANZANIA YASAINI MAKUBALIANO MKUTANO WA ITU PP 2022

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amesaini nyaraka za mwisho za makubaliano ya Nchi wanachama wa ITU, yaliyoafikiwa kwenye Mkutano Mkuu wa ITU PP22 unaohitimishwa leo Ijumaa Tarehe 14 Oktoba, 2022 jijini Bucharest, Romania.

Shirika la ITU lilikutanisha Nchi wanachama wake mnamo tarehe 26 Septemba, 2022 ambapo pamoja na majadiliano ya Kisekta, Tanzania ilichaguliwa kuwa miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la ITU kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2023 hadi 2026.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!