Home Kitaifa TANZANIA YAPATA BILIONI 3.3 KWA KUUZA LITA 272, 444 ZA VIUATILIFU VYA...

TANZANIA YAPATA BILIONI 3.3 KWA KUUZA LITA 272, 444 ZA VIUATILIFU VYA KUUA MAZALIA YA MBU – DKT. KIJAJI

TANZANIA imepata kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kwa kuuza lita 272, 444 za viuatilifu vya vya kuua mazalia ya mbu kupitia kiwanda cha Tanzania Biotech Products Ltd (TPBL).

Hayo yalisemwa na Dk Ashatu Kijaji wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea mafanikio mipango na mikakati ya kiwanda hicho cha (TPBL) kinachojihusisha kuzalisha viwatilifu vya kuuwa mazalia ya mbu ambacho kiko chini ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Amesema kuwa dawa hiyo imeuzwa kwenye nchi saba za Afrika za Kenya, Angola, Niger, Botswana, Namibia Msumbiji na Swatini huku mazungumzo na nchi ya Uganda ikiwa kwenye mazungumzo ya kununua dawa hiyo.

“Tunataka hii ndiyo iwe bidhaa itakayoitangaza Tanzania kwa kuuzwa nchi jirani na Afrika nzima kupitia eneo huru la biashara ambapo kuna nchi 54 ambapo bidhaa zitaingia kwenye soko hilo bila ya kodi na tozo ambapo majadiliano bado yanaendelea,” amesema Kijaji.

Aidha amesema kwa sasa baada ya viuatilifu hivyo kupata soko kubwa na uzalishaji wa viuatilifu hai ambavyo vitatumika kwenye kilimo vimeonekana ni vizuri na tayari mamlaka udhibiti mimea imetoa cheti cha usajili.

“Nataka uzalishaji uongezeke kuanzia Oktoba ili kuwahi msimu wa kilimo unaokaribia kuanza ili iingie sokoni na uzuri haina kemikali kwani ni rafiki kwa afya na mazingira na ni vema ikatumika kwenye mpango wa BBT tutaongea na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa ajili hiyo,” amesema Kijaji.

Amesema kuwa anatoa siku tano kwa Shirika la Viwango Nchini (TBS) kukamilisha ithibati ya ili dawa hiyo iwe kwenye viwango vinavyotakiwa pia itambuliwe na viwango vya kimataifa ISO ili nchi iweze kuhudumia dunia kwa kilimo kwani matumizi ya viuatilifu hivyo ni salama kwa chakula.

“Kitengo cha masoko kijiangalie kwani kiwanda kinapaswa kijiendeshe kwani ni cha kibiashara siyo cha huduma kwani kinatakiwa kizalishe bidhaa bora serikali ipate mapato nataka taarifa ndani ya siku 14 nipate majibu na hatutatoa tena maelekezo bali tutakuwa tofauti,” amesema Kijaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Dk Nicoluas Shombe amesema kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalishaji wa dawa hiyo ni milioni sita kwa mwaka.

Shombe amesema kuwa kiwanda hicho ambacho kilianza uzalishaji mwaka 2017 kilianzishwa kwa malengo ya kukabiliana na ugonjwa wa maleria kwa kuua mazalia ya mbu ili ifikapo 2025 maambukizi yawe 0 na cha kipekee Afrika na duniani vikiwa ni vitatu tu kikiwa kinazalisha dawa za kibaiolojia.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Dk Lugano Wilson alisema kuwa maelekezo yote yaliyotolewa watayafanyia kazi ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Wilson amesema kuwa azma ya serikali ni kupambana na kuutokomeza ugonjwa huo kwa kuua mazalia ya mbu.
++++++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!