Home Biashara TANZANIA NA MSUMBIJI KUFANIKISHA USHIRIKIANO SEKTA YA BIASHARA

TANZANIA NA MSUMBIJI KUFANIKISHA USHIRIKIANO SEKTA YA BIASHARA

Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Mhe. Silvino Augusto Jose Moreno, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Msumbiji kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Jijini Maputo.

Katika mkutano huo, Viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ili kufanikisha ushirikiano katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji.

Vilevile, Viongozi hao wamekubaliana kutafuta mbinu na mikakati mahsusi ya kuongeza kiwango cha biashara baina nchi hizi ili kiende sambamba na uhusiano wa kindugu, kihistoria na kijiografia baina ya nchi hizi.

Moja ya maeneo yaliyopendekezwa ni kuanzisha Jukwaa la Pamoja la Biashara litakalowakutanisha Wafanyabiashara na wadau wengine muhimu ili kubadilishana uzoefu, kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na kubaini namna ya kunufaika nazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!