Home Kimataifa TANZANIA NA MISRI WAKUBALIANA KUENDELEA NA MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA NA MABWAWA.

TANZANIA NA MISRI WAKUBALIANA KUENDELEA NA MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA NA MABWAWA.

Cairo-Misri

Mapema Tarehe 16 Octoba Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso alikutata na Waziri wa Maji wa Misri Mhe.Profesa Nabhan Sweilam Jijini Cairo na kuelekeza timu ya wataalamu aliyeambatana nayo kukutana haraka na kukubaliana namna ya kuendelea na Mradi wa uchimbaji wa Visima 30 na ujenzi wa Mabwawa mawili (2) uliokwama kutekelezwa na Serikali ya Misri nchini Tanzania.

Kufuatia maagizo hayo ya Mhe.Aweso.mapema tarehe 18 Octoba.2022 Jijini Cairo wataalamu wa Tanzania wakiongozwa na Dkt.George Lugomela ambaye ni Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji-Wizara ya Maji wamekutana na timu ya majadiliano kutoka Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji ya Misri wakiongozwa na Mkurugenzi Dkt.Mamdouh Hassan na kujadili kwa kina mradi wa uchimbaji visima virefu 30 na ujenzi wa mabwawa makubwa mawili ambao utekelezajii wake ulikuwa umekwama kwa muda mrefu.

Aidha wataalamu hao wamekubaliana juu ya hatua za kuchukua ili kukwamua mradi huo na kuendelea kubainisha mipango ambayo inakubalika kwa pande zote mbili,makubaliano yaliyofikiwa yatawezesha kuendelea kwa hatua za kuwekwa saini kwa mkataba wa ujumla wa ushirikiano wa kiufundi (framework Agreement) ambao utawezesha utawezesha wataalamu wa Nchi ya Misri kuja Tanzania na kufanya kazi na wataalamu wa hapa ili kuweza kuandaa vizuri zaidi mradi huo na kufikia gharama halisi ya mradi kabla ya kuwekwa saini kwa mkataba wa Fedha ambao utawezesha utekelezaji wa mradi kuanza haraka iwezekanavyo na kusaidia maeneo yenye changamoto kubwa ya maji nchini yanayohitaji Visima na Mabwawa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!