Home Kitaifa TANZANIA NA MALAWI KUSAINIA MKATABA MAKUBALIANO WA USHAROBA KUPITIA BANDARI YA DAR...

TANZANIA NA MALAWI KUSAINIA MKATABA MAKUBALIANO WA USHAROBA KUPITIA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Na Magrethy Katengu

NCHI ya Tanzania na Malawi zimewekeana saini ya mkataba wa ushirikiano kuhusu usharoba wa usafirishaji bidhaa baina ya nchi hizo mbili huku ikielezwa Malawi itatumia Bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema Malawi ni Mtumiaji wa bandari ya Dar es salaam hivyo kupitia mkataba huo Ushirikiano wao utaimarika na kwani pia SGR nayo itahusika katika usafirishaji mizigo

Kwa kuwa mkataba huu ulikuwepo wa muda mrefu na tumesainiana upya kwa lengo la kuhakikisha sasa unafanya vizuri zaidi kwani Serikali imejenga miundombinu mingi kwaajili ya kuboresha ushoroba huo wa usafirishaji kati ya nchi hizo mbili, ” amesema.

Hata hivyo amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanya maboresho makumbwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kuanzia gati namba moja hadi namba saba huku uwekezaji ukitarajiwa kufanyika akifafanua kuwa wamejenga gati maalum kwaajili ya gati namba zero.

Sanjari na hayo katika kuendeleza uwezo wa bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha utoaji huduma ndio maana wameamua kutoa nafasi kwa sekta binafsi kufanya uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kusisitiza wanafanya hayo yote kuhakikisha wanaongeza ufanisi kwa ajili ya bandari hiyo.

Akizungumzia Bandari ya Mtwara Profesa Mbarawa amesema Serikali amefanya mabadiliko makubwa ikiwemo kujenga gati la kisasa mbali na urefu takribani mita 300 inafanya kazi na wameweka vifaa vya kisasa.

Pia amesema wiki inayokuja wanatarajia kusaini mkataba kwaajili ya ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay ambayo ni muhumi kwa wakazi wa Ziwa Nyasa.

Bandari hii ni muhimu kwaajili ya watu wa Malawi na jitihada zote zinafanywa kuhakikisha wanafungua usharoba huo kati ya Tanzania na Malawi

Pamoja na mambo mengine imeelezwa kwa upande wa Malawi utarahisisha upatikanaji wa bidhaa kwa nchi yao wakitumia korido ya Mtwara ambayo itapunguza gharama ya usafirishaji bidhaa na hivyo wananchi kupata bidhaa kwa bei nafuu.

Akizungumzia faida ya mkataba huo, Profesa Mbarawa amesema mkataba huo unafaida kwa Tanzania na Malawi huku akieleza kwamba kwa mwaka 2022 mzigo ulihudumiwa na bandari ya Dar es Salaam kwa nchi ya Malawi ulikuwa takribani ya zaidi tani 500, 000

Lakini ukilinganisha na mwaka 2018 kumekuwa na ongezeko kubwa hivyo tunataka ongezeko lifikie hadi tani million moja au mbili na hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam

Tumekuwa tukisaini mikataba kwaajili ya kuifungua Bandari ya Dar es Salaam japo kuna ushindani na tukipanga vizuri kama tunavyoendelea na ujenzi wa miundombinu hakuna mtu ataweza kushindana. Kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi na Kazi za Umma nchini Malawi Jacob Hara ametumia nafasi hiyo kuelezea manufaa ambayo yanakwenda kupatikana kwa nchi zote mbili baada ya kusaini mkataba huo Jacob unaotoa fursa kwa nchi yao kutumia bandari ya Dar es Salaam.

Aidha amesema anaamini mkataba huo waliousaini utasaidia kufanya kazi kwa pamoja kati ya Tanzania na Malawi na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwa gharama nafuu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!