Na Shomari Binda-Musoma
TANZANIA imekusudia kuimalisha zaidi usalama wakati wa matumizi ya usafiri majini kwenye bahari na ziwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ( SMZ ) Khalid Muhamed Salum kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Usafiri wa Majj Duniani na miaka 50 ya uanachama wa IMO.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Makame Haji kwenye ufunguzi uliofanyika kitaifa leo septemba 23 uwanja wa shule ya msingi Mukendo.
Amesema suala la usalama lina umuhimu mkubwa na kutaka maadhimisho hayo yatumike kukumbushana na kuzingatia usalama.
Makame amesema Tanzsnia kama nchi mwanachama wa Mamlaka ya Bahari Duniani ( IMO ) inazingatia mkataba wa mamlaka hiyo na usalama unasisitizwa.
Amesema usafiri wa majini ni moja ya usafiri unaotegemewa hivyo ni muhimu wananchi kupata elimu juu ya usalama.
” Hii ni siku muhimu kupitia maadhimisho haya kukumbushana suala la usalama tunapotumia vyombo vya usafiri wa majini kwenye bahari na ziwa.
” Maeneo ya maji ni muhimu kwa uchumi kupitia uvuvi na uchumi wa buluu ambao unatangazwa na kuhimizwa kwa sasa”,amesema.
Naibu Katibu mkuu huyo kwa niaba ya Waziri Kharid ameishukuru serikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza zaidi kwenye bahari na maziwa kwa kutengeneza meli na miundombinu kuinua uchumi.
Amesema serikali imetengeneza meli 8 kati yake 4 kwa Tanzania bara na 4 visiwani Zanzibar kwaajili ya kuimalisha usafiri wa abilia na mizigo.
Aidha amemshukuru Rais wa Zanzibar Dk.Hussen Mwinyi kwa uwezeshaji uchumi wa buluu na muongozo mzuri wa usimamizi wa matumizi ya bahari.
Mkuu wa chuo Bahari ( DMI ) Dkt.Tumaini Gurumo amesema kupitia chuo hicho wataendelea kutoa mafunzo yanayozingatia usalama ili usafiri wa majini uendelee kuimalika.
Akitoa salamu za mkoa wa Mara kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kanali Evans Mtambi,Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Gerald Kusaya amewakaribisha wadau wote kwenye maadhimisho hayo na kusema mkoa upo salama na wananchi wayatumie maadhimisho hayo kujifunza.
Maadhimisho ya Siku ya Usafiri wa Maji Duniani na Miaka 50 ya Uanachama wa IMO kitalifa yanafanyika mkoani Mara yakiwa na kauli mbiu isemayo ” Mustakabali wa Uboreshaji wa Usafiri Majini Usalama Kwanza”.