Home Kitaifa TANZANIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VIVUKO KUHAKIKISHA USALAMA BARABARANI

TANZANIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VIVUKO KUHAKIKISHA USALAMA BARABARANI

VILABU vya Kimataifa vya Usalama barabarani (ACTA) yafunga mafunzo yaliyofanyika kwa siku tatu, jijini Dar es Salaam huku wakihaidi kuboresha Miundombinu barabara korofi karibu na shule za Jiji la Dar es Salaam.

Lengo la mafunzo hayo ni kuangalia viwango vya barabarani zilizopo katika nchi mbalimbali za Afrika, kupunguza ajali na vifo hususan kwa watoto wa shule.

Nchi zilizoshiriki mafunzo hayo ni Tanzania ambao ndiyo mwenyeji, Kenya, Botswana, Namibia, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini na Uganda.

Akizungumza baada ya kufunga mafunzo hayo Mwakilishi wa Tanzania, Najma Rashid amesema katika nchi zilizoshiriki Namibia ndio nchi pekee kwa msaada wa klabu yao ya Usalama Barabarani imeboresha Miundombinu kiasi kwamba imekuwa na takwimu ndogo ya Ajali na vifo .

Tanzania tunashukuru usalama wa barabarani upande wa shule tunafanya vizuri hakuna kesi za ajalie kama kipindi Cha nyuma, lakini bado hatujafikia kiwango kikubwa kama Namibia”

Mwakilishi huyo ameeleza kuwa wanashukuru serikali wanatoa sapoti ikiwemo kutengeneza barabarani zenye viwango ambavyo zinapunguza ajali.

“Washiriki wote ambao walikuwepo katika mafunzo wataenda kuwa mabalozi wazuri kwa nchi zao na kuhakikisha bajeti itakayowekwa itaenda kuweka mikakati kwa namna watakavyoweza kusaidiana na serikali kujenga na kuboresha miundombinu barabarani,” alisema.

Mwenyekiti wa Shirikisho la klabu za usalama wa barabarani (ACTA) kutoka nchini Botswana, Simon Mang amesema dhumuni la mafunzo hayo ni kuzipa uwezo wawakilishi wa mataifa uelewa namna ya kufanya utetezi na kushirikiana na serikali katika kushughulikia masuala ya usalama barabarani Afrika na kuona namna ya kuboresha miundombinu.

“Nilikua sehemu ya maandalizi na nilikuwa sehemu ya mshiriki na Mjumbe katika mkutano huo ambapo tulijadili kuomba ruzuku kutoka Taasisi ya (FI ) Kuomba ruzuku ya kufanya kampeni ya Helmenti na kufanya mafunzo ya udereva wa usalama kwa madereva wa mabasi, “alisema Mang.

Mang aliwaomba serikali wa nchi za Afrika kuhakikisha wanaunga mkono mashirikisho hayo yanayolenga kuhakikisha usalama wa barabarani kwani watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kutokana na miundombinu mibovu iliyopo.

Hata hivyo wawakilishi hao wa klabu walipata nafasi ya kutembelea shule ya Wailes Wilaya ya Temeke kuona namna miundombinu ilivyoboreshwa na kuwa rafiki kwa watoto wa aina zote ikiwemo walemavu ambapo alama ziwekwa kwa ajili yao kuwawezesha kuvuka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!