Ubalozi wa Italia kushirikiana na ubalozi wa Tanzania umeandaa kongamano la kibiashara ( ITALY- TANZANIA BUSINESS AND INVESTMENT FORUM ) lenye lengo la uwekezaji kwenye sekta ya biashara nchini Tanzania Kongamano hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania nchini Italia Mohmoud Thabit Komba amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuekeza sana kwenye kilimo Cha biashara kwa lengo la kukuza na kundeleza viwanda vyetu vya mazao kama vile matunda. Ili mazao yawe yanapatikana kwa urahisi sio mpka kipindi cha msimu.
Pia Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi amesema lengo la kongamano hilo ni kuunda, kuboresha na kuendeleza uhusiano wa kiuchumi baina ya Italia na Tanzania.Pia kupitia uhusiano huo umesaidia kufanikisha uchumi wa Tanzania kukua zaidi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kituo Cha uwekezaji John Mnali ameelezea kuwa takribani kampuni 27 zimekuja Tanzania kwa lengo la kutafuta fursa za biashara na uwekezaji nchini. Wadau hao Wana malengo ya kuwekeza katika sekta tofauti kama nishati,viwanda,kilimo na utalii.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uwekezaji Fadhili Chilumba amesema wizara ya imekuja kuwahakikishia wawekezaji kuwa wanaekeza katika sehemu salama maana Tanzania ni Nchi ya amaniamani na yenye usalama wa kutosha.