Home Kitaifa TANZANIA COMMERCIAL BANK (TCB) YAZINDUA KAMPENI KABAMBE YA KIKOBA KIDIGITALI

TANZANIA COMMERCIAL BANK (TCB) YAZINDUA KAMPENI KABAMBE YA KIKOBA KIDIGITALI

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo, akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa Kikoba Kidigitali uliofanyika leo Mei 9,2024 Jijini Dar es Salaam.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Kufuatia kukua na kuimarika kwa Maendeleo ya Teknolojia nchini kumewezesha wananchi wengi kupata huduma za kibenki kwa njia salama na kuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo, wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Kikoba Kidigitali uliofanyika leo Mei 9,2024 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa uzinduzi huo umelenga kusogeza huduma ya usajili wa kujiunga na Kikoba kupitia mtandao wake wa simu anaoutumia.

Ameongeza kuwa hapo awali huduma hiyo iliwapa fursa wateja wa mtandao mmoja pekee jambo ambalo liliwanyima fursa wateja wa mitandao mingine.

“TCB Benki, imeshirikiana na Kampuni zote za simu nchini zikiwemo, Tigo, Airtel, Halotel na Vodacom, ili kurahisisha namna ya kusajili na kujiunga na Kikoba mtandaoni.

“Ukiwa na Kikoba mtandaoni ni salama zaidi, kwani nirahisi kuona miamala yao, na kuleta uwazi kati ya wanachama” amesema Mihayo.

Amefafanua kuwa hatua hiyo imewezesha kuwa na aina mbili za vikoba, ambapo aina ya kwanza ni kumwezesha mteja kusajili au kujiunga na kikoba kupitia mtandao wake wa simu anaoutumia, na aina ya pili ni M-Koba inayomwezesha mteja kusajili Kikoba na kikundi cha watu wanaotumia mtandao mmoja wa Vodacom.

Awali akitoa neno la utangulizi katika sherehe hizo, Mkurugenzi wa Masoko wa Benki hiyo, Deo Kweyunga amesema kuwa uzinduzi huo utakwenda nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kuwahamisha Kuchangamkia fursa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!