Na Magrethy Katengu,
Dar es salaam.
Bodi za Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) pamoja na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) zimekutana na kuweka mipango na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Mkutano wao Jijini Dar es salaam leo December 4/2023 Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni amesema kuwa mkutano huo una mlengo wa kuendeleza sekta Mafuta na Gesi asilia katika kutafuta wawekezaji.
“Leo hii tumekutana kujadili ,kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu ili tuweze kudhibiti na kuendeleza sekta hii muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu,tunatumaini mara baada ya kikao hiki tutaainisha mikakati yetu na kuifanyia kazi ipasavyo” amesema Mhandisi Sangweni.
Naye Mkurugenzi Mwendeshaji Mkurugenzi Mwendeshaji Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Ges Asilia Zanzibar (ZPRA) Adam Makame amesema mkutano huo una mlengo kuweka mazingira bora kwa pamoja na kutangaza vitalu vya Mafuta na Gesi asilia ili kuweza kupata wawekezaji wengi nakuwezesha kupata kukuza a sekta hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Alfan Alfan amesema kwamba ushirikiano wa PURA na ZPRA kutoka Zanzibar itasaidia kujenga mahusiano ya muda mrefu katika kuhakikisha wawekezaji wanapatikana Tanzania Bara na Visiwani katika ardhi inayopatikana raslimali Mafuta na Ges asilia .
” Ushirikiano huu utaleta manufaa makubwa kwenye bodi zetu hizi mbili( PURA na ZPRA ) kutangaza vitalu vyetu na kupata wawekezaji wengi hivyo sekta ya Mafuta na Gesi asili itazidi kukua nakuleta maendeleo kwa Taifa letu” amesema Alfan
Nae mwenyekiti wa bodi taasisi ya Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Ali Mirza ZNPRA amesema kwamba kikao hicho kimefanyika kwa mara ya kwanza ili kujadiliana kwa pamoja nakuweka mikakati ya pamoja ya kunufaika na rasilimari ya Mafuta na Gesi asilia.