Home Kitaifa TANROADS YATANGAZA TENDA KILOMITA 40 MUENDELEZO UJENZI BARABARA YA MUSOMA-MAKOJO-BUSEKERA

TANROADS YATANGAZA TENDA KILOMITA 40 MUENDELEZO UJENZI BARABARA YA MUSOMA-MAKOJO-BUSEKERA

Na Shomari Binda-Musoma

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS ) imetangaza tenda ya muendelezo wa ujenzi wa barabara ya Musoma-Makojo-Busekera yenye jumla ya urefu wa kilometa 92.

Tenda iliyotangazwa septemba 18/2024 ni kilometa 40 kutoka Musoma hadi Kusenyi yenye kumbukumbu namba TR36/2024/2025/W/33

Hiyo ni barabara kuu na pekee inayounganisha Vijiji vyote 68 ndani ya Kata 21za jimbo la Musoma vijijini na kutegemewa na wananchi.

Akizungumza na Mzawa Blog baada ya kutangazwa kwa tenda hiyo mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema barabara hiyo ni muhimu kwa ukuaji na uimarijaki wa uchumi wa wananchi wa jimbo hilo na taifa kiujumla

Amesema vilevile barabara hiyo ni muhimu sana kwa usambazaji, utoaji na uimarishaji wa huduma za jamii.

“Tunaishukuru sana serikali yetu kutangaza tenda ya ujenzi wa kilomita 40 za barabara hili ambayo ni muhimu kiuchumi kwa wananchi wetu na taifa kiujumla.

“Ujenzi wa awali kilimita 5 za barabara hili ulifanyika kuanzia Kijiji cha Kusenyi hadi Kijiji cha Suguti (Lot II) na huu ni muendelezo wake”, amesema.

Ombi la ujenzi wa barabara hiyo liliwasilishwa kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na mbunge wa jimbo Prof. Sospeter Muhongo hiyo ilikuwa tarehe 6.2.2022, Kijijini Kwibara Kata ya Mugango.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!