Home Kitaifa TANNA YAADHIMISHA MIAKA 51 YA UUGUZI MKOANI TANGA

TANNA YAADHIMISHA MIAKA 51 YA UUGUZI MKOANI TANGA

Na Mwandishi wetu, TANGA.

CHAMA cha Uuguzi Nchini (TANNA) kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Afya kinafanya maadhimisho ya 51 mkoani Tanga ambayo yataanza siku ya Mei 8 hadi 12 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Rais wa TANNA, Alexander Baluhya amesema Mei 8 wanaanza na maadhimisho ya uwasilishaji wa Kisayansi ambapo ni katika kuadhimisha Siku ya Uuguzi Duniani.

“Lengo la maadhimisho haya ni kumuenzi Muasisi aliyeanzisha siku hiyo Bi. Frolence Naitingale ikiwa ni kuhakikisha mwananchi anapata huduma za afya kwa hali ya juu”

“Na hii pia ni katika kurudisha fadhila kwa wateja wetu ambapo kwa kushirikiana na Wadau wetu wa Afya tutaanza kutoa huduma bure kwa wananchi”

Rais Baluhya amebainisha kwamba huduma zinazotolewa ni zile za viashiria vya ugonjwa, lakini pia uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukizwa.

Ameainisha magonjwa hayo kuwa ni shinikizo la damu, kisukari, uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake.

Aidha Rais huyo amewataka wananchi kujitokeza ili kufanyiwa uchunguzi wa nagonjwa mbalimbali ili kujihakikishia usalama wa afya zao.

Sambamba na hayo Rais huyo ameeleza kwamba, “kumekuwa na changamoto ya uwekezaji katika huduma za afya, hivyo basi kupitia maadhimisho haya tunaziomba Mamlaka za Afya kwa mwaka huu kuwekeza katika huduma za afya”.

Naye Katibu Mwenezi wa TANNA Nchini Meshark Makojijo amesema chama kilianzishwa mwaka 1975 kwa lengo la kuangalia na kulinda maslahi ya wanachama wake ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zao.

Makojijo amefafanua kwamba kutokana na huduma za kiuguzi zipo changamoto ambazo zikijitokeza kada ya uuguzi inaonekana haifai kwamba hawafanyi kazi yai ipasavyo.

“Kama TANNA tunamuomba sana Muheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Hassan Suluhu azione huduma za uuguzi ni muhimu zaidi ili wananchi wapate huduma bora zaidi” amesema.

Maadhimisho ya 51 ya Siku ya Uuguzi Duniani kwa mwaka huu yanaadhimishwa Kitaifa katika Mkoa Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!