Home Kitaifa TANESCO YAZINDUA MPANGO WA MIAKA 4 KUONGEZA IDADI YA WAHANDISI WANAWAKE

TANESCO YAZINDUA MPANGO WA MIAKA 4 KUONGEZA IDADI YA WAHANDISI WANAWAKE

Na Magrethy Katengu

Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) limesema litahakikisha linaongeza jitihada ya kuongeza idadi ya Wahandisi Wanawake katika fani hiyo ili kusaidia utekelezaji wa Mlengo wa Jinsia sawa kwa wote na kusaidia kufikia dira ya Dunia asilimia hasini kwa hamsini kwa wote katika kuchochea Uchumi wa Maendeleo endelevu .

Ameyasema hayo Januari 29, 2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme TANESCO Mhandisi Gisima Nyamo_Hanga katika hafla ya Uzinduzi wa Mpango maalum uwezeshaji inayolenga kuwajengea uwezo wahandisi wanawake, kuwaendeleza kiujuzi na kielimu,kwa lengo la kuongeza ushiriki wao katika shughuli za uendelezaji miradi nchini.

Mkurugenzi Tanesco Mhandisi Nyamo_Hanga amesema,Mpango huo ni wa miaka minne na watashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT),ambavyo watavitumia Vyuo hivyo kuwaendeleza kielimu wataalamu wakike washirika hilo, kusaidia kuwapata wanafunzi wanaohitimu fani ya uhandisi.

“Wahandisi wanawake katika sekta ya Umeme Ushiriki wao bado ni mdogo na sisi kama TANESCO tumeona ni muhimu kuja na mkakati maalum ambao utasaidia kuongeza wahandisi wengi wa kike ambao tutawaajiri na kufanya nao kazi kwani tunaamini mwanamke akipata elimu na akikabidhiwa na kupewa imani kufanya jambo lolote anafanya kwa uaminifu mkubwa na mafanikio makubwa mfano tunauona na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani” amesema Mkurugenzi Tanesco

Hata hivyo Mkurugenzi amebainisha kuwa Mradi huo unaratibiwa na Umoja wa Ulaya, lakini mpango wao wa mbele ni kuhakikisha kwamba unakua endelevu na hata baada ya huo mradi kuisha wao wenyewe wataendelea kuweka jitihada za kuendelea, lengo ni kuwapata wahandisi wengi wakike .

Ameongeza kwa kusema kuwa mradi huo umeanza na wanawake 40 ambao wanawezeshwa kielimu katika vyuo vikuu vya ndani na programu hiyo itakua ni ya miaka minne hivyo rai kwa wahandisi wakike kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika mpango huo.

“Mradi huo ni moja ya kichocheo cha kuwahamasisha watoto wakike kusoma fani ya uhandisi, mradi huu tumeanza na wanawake 40 lakini kila mwaka tutakua tunaongeza wengine,” amesema.

Kwaupande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Seif Shekalage, amesema hiyo programu iliyoanzishwa ni.jitihada ya kusaidia kuwapatia elimu.wanawake na kuwanufaisha kiuchumi wanawake ili nao waweze kuwa katika nafasi nzuri serikalini
.

Amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maluum ipo tayari kushirikiana na TANESCO ili programu hiyo iwe mfano bora na wa kuigwa na taasisi na mashirika mengine nchini.

Naye mnufaika wa programu hiyo Mhandisi Catherine Mwigoha kutoka TANESCO,ameshukuru sana kupata.fusa hiyo kupitia mradi huo utasaidia kuwaongezea ujuzi,ambao utawezesha kuongezeka kwa uzalishaji ndani ya shirika hilo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!