Home Biashara TANESCO REA ZASHAURIWA KUNUNUA TRANSFORMA TANALEC, GENERAL TYRE KUFUFULIWA

TANESCO REA ZASHAURIWA KUNUNUA TRANSFORMA TANALEC, GENERAL TYRE KUFUFULIWA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) ametoa rai kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuongeza kasi ya ununuzi wa transfoma zinazozalishwa na Kiwanda cha Tanelec kwa kuwa Taasisi hizo ni wamiliki wa sehemu ya hisa za kiwanda hicho ili kukiwezesha kiendelee kukua na kuongeza ajira nchini.

Dkt Jafo ameyasema hayo Agosti 24, 2024, Mkoani Arusha, alipotembelea viwanda, kuongea na Wafanyabiara pamoja na Maafisa Biashara wa Mkoa huo kwa lengo la kujionea shughjuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto na kuona njia bora ya kuzitatua kwa kushirikiana na Taasisi nyingine husika ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Aidha, Dkt Jafo amelielekeza Shirika la Taifa la Maendeleo NDC kuhakikisha linapata mwekezaji makini kwa ajili ya Kiwanda cha Matairi cha General Tyre East Africa (GTEA) Limited ili kifufuliwe na kuanza uzalishaji wa matairi lengo la kuongeza ajira na patonla taifa kwa ujumla

Katika hatua nyingine akiongea na Wafanyabiashara, Wamiliki wa Viwanda na Maafisa Biashara wa Mkoa wa Arusha, Waziri Jafo ametoa rai kwa Watanzania kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa sekta ya viwanda na biashara inasonga mbele kwa kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha mazingira ya biashara ikiwemo miundombinu ya maji, barabara, reli, umeme na matlrekebisho mbalinbali ya Sera Sheria na Kanuni.

Aidha, Dkt Jafo amebainisha kuwa akiwa Mkoani humo ametembelea
Kiwanda cha Maziwa cha Tanzania Dairies Limited (TDL), Kiwanda cha Kilimanjaro Textile Mills Limited (Kilitex), Kiwanda cha General Tyre East Africa (GTEA) Limited, Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited, Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha TANELEC Limited, Kiwanda cha nguo cha Sunflag na Kiwanda Moonlight Tanzania Limited

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ameaidi kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na TAMISEMI ili kuhakikisha changamoto zote za wafanyabiashara zinatatuliwa kwa hatua ili kuhakikisha viwanda vyote mkoani humo vinafanya kazi na Mkoa wa Arusha unakiwa Mkoa wa Mfano katika kuendeleza viwanda na kukiza biashara.

Naye Mkurugenzi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe amesema NDC imepokea maelekezo yote na itayafanyia kazi ilinkuhakikisha kiwa kiwanda cha General tiyre kinafuguka na kufanya kazi kwa ufanisi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!