Na Boniface Gideon, TANGA
IDADI ya watanzania wanaotembelea hifadhi mbalimbali zilizopo hapa nchini zinazo simamiwa na shirika la hifadhi ya Taifa ‘TANAPA‘ inazidi kuongezeka kadiri siku zinavyokwenda hii ikichangiwa zaidi na elimu inayotolewa sambamba na hamasa iliyopatikana kufuatia uzinduzi wa Royal tour uliofanywa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan nchini Marekani mwaka 2022..
Hayo yamebainishwa na Ofisa Utalii kutoka hifadhi za Taifa ‘TANAPA‘ Athumani Mbae wakati akizungumza katika maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga ikiwa ni ya 10 yakihusisha taasisi na makampuni ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali wajasiriamali wakubwa, wa kati na wadogo wadogo , yakiwa na lengo la kutangaza biashara na huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Mbae lisema hifadhi zote zinazosimamia na TANAPA zimekuwa zikipata watalii wengi wa ndani na nje hii ikisadifu matokeo na hamasa kubwa iliyopatkana kupitia filamu ya Royal tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni jitihada za serikali ya awamu ya 6 kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia sekta ya utalii.
“Kwa kweli utalii unakuwa siku hadi siku na hii inayokana na juhudi kubwa ambazo zinafanywa na shirika la hifadhi za Tanzania “TANAPA” lakini pia kupitia Royal tour ambayo alizindua Rais Samia Suluhu Hassan amefanya juhudi kubwa kuzitangaza hizi hifadhi tangu ametoa filamu hiyo utalii umekuwa na tumejulikana sana kimataifa tunapata wageni wengi kutoka nje lakini pia na watalii wa ndani na hata watanzania wenyewe wamekuwa na muamko kwa kuona kwamba Rais wetu anaweka juhudi kubwa katika sekta ya utalii” alisema Mbae.
Aliongeza kuwa licha ya ongezeko la watalii wa ndani na nje katika hifadhi zilizopo kumekuwa na changamoto ya miundombinu mibovu hasa kipindi cha mvua barabara zimekuwa hazipitiki kiurahisi hata hivyo serikali iliona hilo ambapo ilitoa fedha kwaajili ya ukarabati wa barabara zote ili kuhakikisha zinapitika kiurahisi.
” Changamoto kama ya miundombinu wakati wa masika inakuwa na shida kwamba ufikikaji wa maeneo ya hifadhi kidogo barabara zinaleta shida lakini serikali inaleta fedha nyingi za kurekebisha hizo barabara kwa sasa hivi barabara zote zinapitika kwa muda wote“alisema mhifadhi huyo.
Alisema kupitia maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka mkoani Tanga kumekuwa na tija kwa upande wa TANAPAambapo wanayatumia kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuvijua vivutio vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini na faida ya kuvitembelea.
“Ni fursa ya kipekee kupitia maonyesho haya kuzitangaza hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa wakazi wa Tanga lakini pia kwa watanzania wote kuvijua vivutio mbalimbali vilivyopo kuwafanya kuzielewa hizi mbuga ziko wapi , vivuyio vilivyopo , shughuli zinazofanyika, huduma zinazopatikana na faida zake ” aliongeza.
Shirika la hifadhi ya Tanzania ‘TANAPA‘ linalosimamia hifadhi takribani 22 hapa nchini zikiwemo Mkomazi, Mikumi , Saadan, hifadhi ya Nyerere, na nyinginezo linaendelea kuwakaribisha watanzania (watalii wa ndani ) kwenda kutembelea na kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana ambapo oiinhilio ni shilingi elfu tano Mia nne(5,900) kwa watalii wa ndani..
Mwisho