OR -TAMISEMI
Menejimenti wa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakiongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe wamemuaga aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Innocent L. Bashungwa ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu wa Wizara yaliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma Leo tarehe 06 Oktoba 2022.
Hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi wa Wizara hiyo ikiwa ni pamoja na Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Afya), Mhe. David Silinde, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara hiyo.
Ikumbukwe kuwa tarehe 02 Oktoba, 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumteua Mhe. Angellah J. Kairuki kuwa Mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI
Pia, Mheshimiwa Rais alimteua Mhe. Innocent L. Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambapo awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).