Home Kitaifa TAMASHA LA VIJANA WA VYUO VIKUU KUKUSANYA VIJANA TAKRIBANI ELFU 30

TAMASHA LA VIJANA WA VYUO VIKUU KUKUSANYA VIJANA TAKRIBANI ELFU 30

Na. Magreth Mbinga

Umoja wa vijana wa vyuo vikuu Jimbo kuu la Dar es Salaam wameandaa mkesha mkubwa uliobeba jina la usiku wa sifa wenye lengo la kuombea Taifa, kusifu, kubudu na kumshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka salama.

Hayo yamezungumzwa na Paroko wa parokia ya Mburahati na Mkurugenzi wa Utume wa Walei Padre Vitalis James Kasembo katika mkutano na Waandishi wa habari ambao umelenga kuwataarifu vijana kushiriki Mkutano huo.

Maisha ya wanadamu kwetu sisi wakristo hasa wakatoliki ni kama mkesha tunakesha ili kusubiri kile Mungu ambacho ametuandalia na tunakumbushwa sisi wakatoliki kwamba kuna maisha kabla ya kuondoka hapa Duniani” amesema Padre Kasembo

Pia Padre Kasembo amewaalika vijana wote wa vyuo vikuu kushiriki mkesha huo na kuwahasa wazazi kuwaruhusu vijana waweze kushiriki ili kujifunza mambo ya Mungu kwa upande wao.

Aidha Mratibu wa Utume wa Walei Karismatiki Jimbo Katoriki la Dar es Salaam Ludovick Maina Kawishe amesema wanazo huduma mbalimbali katika unjilishaji hasa katika Vyuo ambapo mwanzoni walikuwa wanatumia Utume wa vyuo vikuu na sasa wamerekebisha kwa kuchanganya vyuo vyote hata ambavyo sio vyuo vikuu. No

Ninafasi ya pekee kuwainjilisha vijana sababu vijana watapata nafasi ya kuhudhuria maadhimisho ya Misa ambayo itaadhimishwa na Baba Askofu Yuda Tadeus Rwaichi ambayo itaanza saa tatu usiku” amesema Kawishe

Sanjari na hayo Mratibu wa maandlizi ya mkesha wa usiku wa sifa Ronaldo Robert Chota amesema mkesha utafanyika ijumaa ya Disemba 16 ,2022 kuanzia saa 3 kamili usiku hadi saa 11 alfajiri na watu wataanza kuingia uwanjani saa 12 jioni na hautakuwa na kiingilio.

Kwa wanafunzi wote wa vyuo vyote vikuu na vyakati kama 51 ambavyo tumevifikia kunamagari kutoka katika kila Chuo kuanzia saa 11 magari yataanza kutoka kuelekea uwanjani” amesema Chota

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!