Home Kitaifa TAMASHA LA USAMBARA TOURISM FESTIVAL LASOGEZWA MBELE

TAMASHA LA USAMBARA TOURISM FESTIVAL LASOGEZWA MBELE

Na Ashrack Miraji Lushoto Tanga

Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Mkoani Tanga,Jafar kubecha amewaomba radhi wananchi na wageni wote waliotarajia kuja kwenye tamasha la kitalii la “Usambara Tourism Festival” lenye lengo la kukuza uchumi hasa kwenye sekta ya utalii wilayani hapo.

Kubecha amesema tamasha hilo ambalo lilipagwa kufanyika Julai 25-27 mwaka huu kuwa limesogezwa mbele kutoka na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao,hivyo tamasha hilo litafanyika Septemba 6 – 7 mwaka huu.

“nitumie fulsa hii kuwapa pole wananchi na wageni wetu ambao tuliwatarajia kushiriki kwenye tamasha letu kuja kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii na majengo makubwa ambayo yalijegwa na mjerumani hususani jengo la Mkuu wa Wilaya ya Lushoto” alisema Kubecha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!