Home Kitaifa TAMASHA LA SAMIA FASHION FESTIVE KULETA FURSA KWA WABUNIFI MAVAZI

TAMASHA LA SAMIA FASHION FESTIVE KULETA FURSA KWA WABUNIFI MAVAZI

Na Magrethy Katengu
Dar es salaam

Wabunifu wa mavazi nchini wameshauriwa kutumia fursa zinazojitokeza kuonesha kazi zao wanazozifanya ili waweze kujulikana na kuinuka kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa Dar es salaam Oktoba ,2024 Muanzilishi na Muandaaji wa Tamasha la Samia Fashion Festival Khadija Mwanamboka wakati akitoa taarifa juu ya TAMASHA la Samia Fashion Festival kuja kivingine kutoa fursa ya linatarajiwa kuanza Oktoba 27,2024 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam ambapo watoto wataanza kwa kuvaa nguo zilizobuniwa na wabunifu.

Mwanamboka amesema kwamba tamasha hilo litahusisha watoto kuanzia umri wa miaka 7 Hadi 17 ili waweze kuonyesha vipaji vyao na maavazi waliyovishwa na wabunifu.

“T amasha hili limepewa jina kwa heshima ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na maono yake na ni heshima kwa uongozi wake katika kukuza utamaduni wa Tanzania kupitia mavazi hasa katika sekta ya ubunifu” amesema

“Tamasha hili limepewa jina kwa heshima ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na limelenga kukuza utamaduni wa Tanzania kupitia mavazi Hulu likionyesha mchango wa Rais katika sekta ya ubunifu.Tamasha litaendelea kwa siku Saba,likijumuisha matukio mbalimbali ya kuwawezesha wanawake,watoto na vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar”,amesema

Aidha kauli mbiu ya tamasha hili ni”Ubunifu na Stara” ikiwa ni taswira tosha ya nafasi na haiba ya mama yeti mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na kwa jinsi Gani jamii inaweza kutumia haiba hiyo yenye stara katika nyanja mbalimbalo za kijamii kama vile motiko,sherehe ,shughuli za jioni ,malezi na kadhalika.

“Tamasha hili si sherehe ya mavazi tu, ni jukwaa la kuonyesha ubunifu wa Kitanzania na ni heshima kwa uongozi na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan “,amesema Khadija Mwanamboka .

Aliongeza kwamba anawakaribisha wabunifu wote kwa mikoa yote ya Tanzania kushiriki fursa hii kwa kutuma kazi zao na jopo la majajo mahiri na wazoefu katika sekta ya mitindo wakiongozwa na Chief Judge mwanamitindo Miriam Odemba ,Mwanamitindo wa Kitanzania anayeishi Ufaransa.

Naye Mbunifu Martini Kadinda ameaema ameguswa na tamasha la Samia festive kushirikisha watoto kwan
jambo zuri la kuwafanya watoto kushiriki Samia Festive hivyo amewaomba wazazi watoto waje kwani hakuna kiingilio

Aidha Tamasha hilo kilele chake inatrajiwa kuwa Zanzibar ambapo waahindi watatu watatu watapewa.zawadi mbalimbali

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!