Home Kitaifa TAKUKURU YABAINI VIASHIRIA VYA RUSHWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO 1800 YENYE...

TAKUKURU YABAINI VIASHIRIA VYA RUSHWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO 1800 YENYE THAMANI YA YRILIONI 7.7

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana an Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni amesema mwaka wa fedha 2022/2023 taasisi hiyo imebaini viashiria vya rushwa kwenye miradi ya maendeleo 1800 yenye thamani trilioni 7.7.

Hayo aliyabainisha jana Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi ya taasisi hiyo kwa mwaka 2022/2023.

Alisema miradi waliyoangalia ni ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko Jiji la Dodoma, mradi wa maendeleo unaotelelezwa kwa kutumia njia ya forced account kwenye Halamshauri ya Jiji la Arusha,mradi wa ujenzi wa soko la wamachinga katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Alisema pia walifuatilia miradi 12 ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji yenye thamani ya sh bil 107.4 katika Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Tabora na Mbeya.

Alisema matokeo ya ufuatiliaji yalionesha uwepo wa mianya ya rushwa ambapo baadhi ya miradi ilionekana kutosajiliwa na bodi ya usajili ya wakandarasi, wakala wa usalama mahala pa kazi, ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi uliosababisha uwepo wa riba.

Pia malipo kufanyika pasipo baadhi ya kazi kufanyika, malighafi za ujenzi kutopimwa ubora wake kinyume na mikataba, ujenzi kufanyika kinyume na matakwa ya mkataba, kutozingatiwa kwa sheria na kanuni za ununuzi wa umma, kuwepo kwa nyongeza ya kazi pasipo kufuata utaratibu.

Alisema kutokana na matokeo ya ufuatiliaji, takukuru ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo marekebisho husika yanafanyika ili kuhakikisha serikali haipati hasara.

Aliongeza kuwa walitoa ushauri wa miradi, kushauri mamlaka husika namna bora ya kuziba mianya ya rushwa ambayo ilibainika.

Alisema katika ufuatiliaji wa miradi 1800, miradi 171 yenye thamani ya sh bil 143,3 ilibainika kuwa na utekelezaji hafifu ambapo uchunguzi ulianzishwa.

Alifafanua kuwa miradi hiyo ilikua katika sekta ya ujenzi, fedha, maji, kilimo pamoja na majengo.

Hamduni alisema walitoa mapendekezo 3668 yalitolewa ili kurekebisha kasoro zilizobainika katika ufuatiliaji huo na kuhakikisha marekebisho kwenye miradi husika yanafanyika kwa gharama za mkandarasi au fedha inarudishwa serikalini.

“Mapendekezo 2740 yalitekelezwa sawa na sawa na asilimia 89.4 ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na takukuru,”alisema.

Alisema Takukuru ilifanya kazi ya uchambuzi wa mifumo 790 ya utoaji wa huduma kwa lengo la kubaini mianya ya rushwa iliyobainika ikiwemo tathmini ya matumizi ya force account katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi.

Alisema tathmini hiyo ilifanyika kutokana an kuwepo kwa changamoto ya utekelezaji wa miradi kwa njia ya forced account ambapo baadhi ya miradi iliyotekelezwa ilikuwa chini ya kiwango, gharama kubwa na kutozingatiwa taratibu za ununuzi.

Alisema kwa ujumla uchambuzi ulibaini baadhi ya watendaji waliokuwa wakisimamia miradi kwa kutumia force account kutokuwa na uelewa au kuwa na uelewa mdogo kuhusu taratibu za manunuzi, ukiukwaji wa sheria na miongozo wakati wa kuunda kamati za usimamizi, ukiukwaji wa sheria wa usimamizi, kutokuwepo kwa mfumo wa udhibiti wa ueledi na taaluma katika utekelezaji wa miradi inayotumia force account.

Pia upungufu wa wataalamu, ukosefu wa fedha za usimamizi wa muda wa utekeelzaji wa miradi, kutokuwepo kwa ukomo wa matumizi ya force account.

Alisema walifanya uchambuzi wa mfumo wa uzingatiaji wa taratibu za ujenzi wa vituo vya mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, uliohusisha vituo vya mafuta 38 na kubaini asilimia 79 ya vituo hivyo kuzingatia sheria ya kuwa na vibaki vya ujenzi kutoka katika Halmashauri ambapo uwekezaji umefanyika.

Alisema asilimia 21 ya vituo vilivyofikiwa havikuwa na leseni wakati wa ufuatiliaji ukifanyika, kuwepo kwa maombi ya ubadilishwaji wa matumizi ya ardhi kutoka yaliyokuwa yamepangwa na kuwa vituo vya mafuta.

Hamduni aliongeza ujenzi wa vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu kuongezeka na kuleta hofu ya usalama kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo hayo,

Alisema katika kuzuia vitendo vya rushwa, takukuru ilibuni takukuru Rafiki inayohusisja mikutano ya wanufaika huduma inayotambua kero katika uitoaji wa huduma au katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo kama hatua hazitachukuliwa zinaweza kusababisha vitendo vya rushwa, manung’uniko katika ngazi hizo.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!