Home Kitaifa TAKUKURU WATAKIWA KUWA WAKALI KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

TAKUKURU WATAKIWA KUWA WAKALI KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Shomari Binda-Musoma

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU ) wametakiwa kuwa wakali kudhibiti vitendo vya Rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava wakati akitoa ujumbe wa mwenge kwenye mkesha kata ya Bukima leo julai 31/2024

Amesema mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji hivyo ni muhimu kujipanga na kuwa wakali kwa watakaopenyeza vitendo vya Rushwa.

Mnzava amesema mtu yoyote anayeomba nafasi ya uongozi kwa kutoa Rushwa sio mtu mzuri na anapaswa kudhibitiwa.

Amesema mwananchi anapaswa kujiuliza mtu anapotoa fedha kuomba uongozi anakuwa na dhamira gani baada ya kuchaguliwa.

” Takukuru muwe wakali sana tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika baadae mwaka huu.

” Tuwadhibiti na kuwabana wale wote watakaopenyeza Rushwa ili wachaguliwe kwenye nafasi za uongozi kwa kuwa watataka kurudisha fedha zao watakapo chaguliwa”,amesema.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa Takukuru pale watakapoona viashilia vya vitendo vya Rushwa.

Mwenge wa Uhuru ukiwa halmashauri ya Musoma umezindua klabu ya wapinga Rushwa kwenye shule ya sekondari Mwibara B na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Takukuru mkoa wa Mara.

Amesema wanafunzi waliopo kwenye klabu hizo wanapaswa kuendelea kupewa elimu ili wawe mabalozi wazuri wa mapambano dhidi ya Rushwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!