Home Kitaifa TAKUKURU PWANI YAONGEZA MAPATO MACHINJIO YA MTAKUJA KIBAHA

TAKUKURU PWANI YAONGEZA MAPATO MACHINJIO YA MTAKUJA KIBAHA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani imefanya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na machinjio ya Mtakuja iliyopo Halmashauri ya Mji Kibaha .

“Uchambuzi huu umefanywa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba kuna mianya ya rushwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ushuru katika machinjio hayo, hali inayosababisha upotevu wa mapato na Halmashauri hiyo hivyo kushindwa kufikia lengo la ukusanyaji waliyojiwekea kutoka kwenye chanzo hiki” amesema.

Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Ally Sadiki alipozungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambao umefanyika leo Aprili 24.

“Uchambuzi huu umebaini kwamba pamoja na kuwepo kwa mashine za kieletroniki za POS katika machinjio kumekua na taarifa zinazokinzana, kuwepo kwa tatizo la miundombinu na ucheleweshaji wa kuweka fedha benki zinazokusanywa.

TAKUKURU imebaini pia kuna uzembe katika kusimamia idadi ya ng’ombe wanaochinjwa kwa siku husika na hakuna ukaguzi kuhusu idadi ya ng’ombe waliopo eneo la kusibiri kuchinjwa.

“TAKUKURU imebaini kuwa idadi ndogo ya watumishi walioajiriwa eneo husika ndiyo chanzo cha kushindwa kutekeleza majukumu ipasavyo” amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Sadiki.

Aidha amesema kuwa baada ya TAKUKURU kuingilia kati makusanyo yameongezeka tofauti na ilivyokua katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kati ya Oktoba na Desemba 2023 ambapo Oktoba hadi Desemba makusanyo yalikua Mil. 7,418,000 na sasa makusanyo yameongezeka na kufikia kiasi cha Mil.9,615,000.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Mji ameongeza watumishi eneo hilo la machinjio ya Mtakuja kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi hivi sasa unafanyika kila mara ili kuondoa fedha za makusanyo ya kila siku na kuhakikisha fedha zinapelekwa benki kila siku

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU amesema kuwa kwa kipindi tajwa wamefanya chambuzi nyingine za mifumo tano katika sekta ya Ardhi, Elimu, AMCOS na ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya serikali ili kupata tija ya mifumo imara usiyokwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza kwa kusema kuwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani wamefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 23 yenye thamani ya Bilioni 6.3 katika sekta za Elimu, Maji, Afya na Ujenzi (Barabara), ambapo kati ya miradi hiyo mradi mmoja umeonekana kuwa na upungufu ufuatiliaji unaendelea ii kurekebisha kasoro hizo.

Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki amesema kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu wameweza kutoa elimu kwa umma kwa kufanya semina 19, mikutano yahadhara21,
vipindi vya redio 9 kuimarisha klabu za wapinga rushwa 54 uandishi makala 4 na TAKUKURU Rafiki.

Aidha TAKUKURU Mkoa wa Pwani imefungua kesi mpya mbili Mahakamani ambapo kesi sita zimeamuliwa huku kesi nne watuhumiwa wametiwa hatiani na jumla kesi sita zinaendelea Mahakamani.

Ameongeza kwa kusema kuwa mikakati waliyojiwekea ni kwamba wamejipanga kuendelea kufanya udhibiti wa mapato ya serikali na usimamizi wa rasilimali za umma ikiwa ni pamoja na udhibiti wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!