Home Kitaifa TAKUKURU NA MISA TAN KUIMARISHA USHIRIKIANO DHIDI YA RUSHWA

TAKUKURU NA MISA TAN KUIMARISHA USHIRIKIANO DHIDI YA RUSHWA

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini Mwa Afrika – Tawi la Tanzania (MISA Tan) Bw. Edwin Soko, amemtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Crispin Francis Chalamila – Januari 20, 2025.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika TAKUKURU MAKAO MAKUU jijini Dodoma, yalilenga kuimarisha ushirikiano katika kuelimisha na kuhabarisha masuala dhidi ya Rushwa pamoja na kuwashirikisha waandishi wa habari kwenye utekelezaji wa Programu ya TAKUKURU RAFIKI.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu amepongeza hatua ya MISA Tan kutaka kushirikiana na TAKUKURU katika jitihada za kuzuia Rushwa na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kwani wadau wa habari wana wigo mpana wa kufikisha habari kwa wananchi.

Mazungumzo hayo yamefanyika ikiwa ni mwendelezo wa uongozi mpya wa Bodi ya MISA Tan ya kuwatembelea wadau mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha na kupanua wigo wa kufanya kazi na wadau hao wakiwemo TAKUKURU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!