Home Kitaifa TAKUKURU MARA YAWATAHADHARISHA WATAKAOENDELEA NA VITENDO VYA RUSHWA

TAKUKURU MARA YAWATAHADHARISHA WATAKAOENDELEA NA VITENDO VYA RUSHWA

Na Shomari Binda–Musoma

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mara imesema itaendelea kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kujihusisha na vitendo vya Rushwa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara Mohamed Shariff wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao ya kipindi cha miezi 3 januari hadi machi 2024.

Amesema katika kipindi hicho ufatiliaji wa miradi 32 yenye thamani ya shilingi 11,372,416,636,.5 katika sekta za afya,elimu,barabara na maji ilifatiliwa.

Shariff amesema katika miradi hiyo ni mradi mmoja wenye thamani ya 4,000,00,000.00 uliokuwa na dosari na hatua zilichukuliwa na zimekuwa na mafanikio.

Amesema katika kipindi hicho pia udatiliaji wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana mkoa wa Mara inayojengwa katika halmashauri ya wilaya ya Bunda yenye thamani ya shilingi bilioni 4,000,000,000 baada ya Takukuru kubaini dosari mbalimbali katika utekelezaji wa mradi huo na hatua mbalimbali zimefanyika kurekebisha mapungufu.

“Kuta ambazo zilikuwa zimepinda kwenye baadhi ya vyumba vya madarasa zimerekebishwa na ‘Expansion joint za mabweni ambazo zilikuwa zimefungwa zimerekebishwa”

“Bweni ambalo plaster imezidi unene tumeshauri fundi akatwe fedha kufidia hasara ya saruji iliyotumika zaidi kwa uzembe wake ambapo alikatwa kiasi cha shilingi 360,000” amesema.

Aidha amesema katika kipindi hicho licha ya shughuli nyingine zilizodanyika uelimishaji umma umeendelea kutolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kifikia taasisi za serikali, binafsi na wananchi ili kuongeza wigo wa mapambano dhidi ya Rushwa.

Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Mara amesema mkakati katika kipindi cha aprili hadi juni ni kuongeza nguvu zaidi kwenye kuzuia vitendo vya Rushwa na kutoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea Rushwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!