![](https://www.mzawa.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250206-WA0088.webp)
Na Shomari Binda-Musoma
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mara imebaini dosari kwenye miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 7,947,792,718.00 katika sekta za afya,elimu,barabara na maji.
Dosari hizo zimebainika baada ya miradi hiyo kufatiliwa kwa kufanyiwa ukaguzi ili kujua ubora wake na thamani ya fedha iliyotumika.
Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara Sadiki Nombo wakati akitoa taarifa kwa umma mbele ya Waandishi wa Habari katika kipindi cha oktoba hadi disemba 2024.
Moja ya mradi uliofatiliwa na kukutwa na dosari ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari Seka iliyopo Wilaya ya Musoma wenye thamani ya shilingi milioni 584,280,029
Katika mradi huo dosari zilizobainika ni kukosa vifaa madhubuti kwaajili ya kusafisha na kusawazisha eneo la ujenzi pamoja na kukosa maji kwaajili ya shughuli za ujenzi.
TAKUKURU katika ufatiliaji wake ilimshauri msimamizi wa mradi kufatilia utaratibu wa kuomba kuunganishiwa maji kutoka ofisi ya meneja wa Wakala wa Maji Vijijini ( RUWASA) na katika utekelezaji tayari wameshaunganishiwa maji.
![](https://www.mzawa.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250206-WA0089-1024x768.webp)
Mradi mwingine ni shule ya sekondari ya wasichana Mara iliyopo wilayan Bunda wenye thamani ya shilingi bilioni 1,450,000,000 ambapo dosari ni kutokujazwa BOQ ya makadilio ya bei ya vifaa.
Licha ya dosari kwenye miradi hiyo na mingine yenye dosari iliyobainishwa kwenye taarifa hiyo,TAKUKURU mkoa wa Mara katika kipindi hicho cha miezi 3 imetekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na utoaji elimu kwa umma juu ya madhara ya Rushwa.
Katika kipindi hicho TAKUKURU mkoa wa Mara imezifikia Kata 25 na kero 126 ziliibuliwa na wadau waliohudhuria vikao vya utoaji elimu na katika kero hoczo 98 zilitatuliwa papo hapo na ambazo hazikupata majibu zilipelekwa idara husika.
Aìdha katika kipindi cha januari na kuelekea uchaguzi mkuu 2025 TAKUKURU itaendelea kudhibiti vitendo vya Rushwa kwa mukibu wa sheria zinazodhibiti vitendo vya Rushwa kwenye uchaguzi.
TAKUKURU mkoa wa Mara Imeendelea kutoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Mara kujiepudha na vitendo vya Rushwa na kushiriki kikamilifu katika kuzuia vitendo vya Rushwa vinavyotokea kwenye maeneo mbalimbali.
![](https://www.mzawa.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250206-WA0091-1024x768.webp)