Na Magrethy Katengu- Dar es salaam
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Kinondoni imesem katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Aprili hadi Juni 2024 imepokea jumla ya malalamiko 88 huku yanayohusu rushwa yakiwa 32 na yasiyohusu rushwa 56.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Agosti 5,2024 Jijini Dar es salaam Naibu Mkuu Takukuru Kinondoni Elizabeth Mokiwa amebainisha kuwa malalamiko ambayo hayakuhusu rushwa waliwaelekeza sehemu sahihi ikiwemo.kwenda kufungu majalada mahakamani na yaliyohusu rushwa yanaendelea kushughulikiwa na yapo katika hatua mbalimbali.
Sanjari na hayo katika kipindi hiko wamefanikiwa kufungua mashauri mapya 16 katika mahakama.ya Wilaya ya Kinondoni na Jamuhuri imeshinda mashauri mawili na mengine yanaendelwa mahakani
Aidha Takukuru Kinondonj imesema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi wajue madhara ya rushwa na washirikiane na Takukuru wanaopoona viashiria vya rushwa dhidi ya viongozi wanaowania uongozi kwani wakiacha rushwa kutumika itawapelekea kupata viongozi ambao siyo waandilifu.