Home Kitaifa TAKUKURU KAGERA YAANZA RASMI KUINADI PROGRAMU YA “TAKUKURU RAFIKI”

TAKUKURU KAGERA YAANZA RASMI KUINADI PROGRAMU YA “TAKUKURU RAFIKI”

Na Theophilida Felician Kagera.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa Kagera tayari imeenza utekelezaji wa uhamasishaji wa programu mpya ya Takukuru rafiki kwa wadau mbalimbali Mkoani Kagera.

Taasisi hiyo imeanza na Madiwani, wakuu wa idara na watendaji wa kata wote wa Manispaa ya Bukoba ambapo zoezi hilo limeanza hii leo mnamo tarehe 5/ mwezi January mwaka huu wa (2023)

John Joseph ni Mkuu wa Takukuru Mkoa Kagera akiinadi programu hiyo kwa wahusika katika ukumbi wa Manispaa hiyo ya Bukoba amesema kuwa mpango huu umeanzishwa mahususi kutokana na maagizo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa malengo yakuitaka Taasisi hiyo kuongeza wigo wa mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Ameeleza kuwa programu hiyo yenye adhima ya kuwafikia kwa ukaribu wananchi katika kuziibua kero zao itawahusisha wadau wote kuanzia wananchi wenyewe, viongozi wa kisiasa wakiwemo Madiwani sambamba na watendaji wa kata wakuu wawilaya wakuu wa mikoa waandishi wa habari na makundi mengine.

Joseph amesema kwamba programu hiyo itasaidia kuzibaini na kuzitatua kero watakazokuwa wamezibaini kwa wananchi kama yalivyomalengo ya Serikali ya kukuza ustawi wa jamii na utawara bora kwa wananchi wake.

“Tutawafikia wananchi kwenye maeneo yao ili watueleze kero wanazokumbana nazo na zitafanyiwa ufumbuzi iwe kwetu sisi au kwa mtu mwingine kwa vyovyote vile zitatatuliwa tuu ndo malengo makubwa ya mpango huu, ndugu zanguni kero hizi ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi wetu zisipodhibitiwa zitaendelea kuzaa madhara makubwa ya rushwa hivyo kupitia programu hii tutaweza kupunguza na kuvidhibiti vitendo vya rushwa” ameleeza Mkuu wa Takukuru John Joseph.

Mbali na hayo amegusia suala zima la madhara ya rushwa hasahasa katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ni kwamba sehemu hiyo nako kumekuwepo baadhi ya watu wasiokuwa wema na kupelekea kuhusisha rushwa maeneo hayo na kusababisha madhara ya kujengwa miradi yenye utofauti na thamani ya fedha husika jambo ambalo amelikemea vikali kwakutoa onyo akiwataka watu wote kuanzia watumishi wa idara zote wakurugenzi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwakuzingatia sheria, kanuni, taratibu na kuzingatia masharti na vigezo vya nafasi walizo nazo.

Kauli mbiu ya programu hiyo John ameitaja kuwa ni “Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu”

Kwa upande wao Madiwani akiwemo Shabani Rashidi kata Bakoba, Brithon Brasio kata Buhembe, Anath Fadhili diwani viti maalumu kata Bakoba wameipongeza sana Taasisi hiyo kwakuja na mpango huo ambapo wameahidi kutoa ushirikiano zaidi katika kuuhamashisha kwa wananchi maeneo ya kata zao kwani unamalengo thabiti yatakayowasaidia wananchi kuyafahamu kwa upana wake madhara ya rushwa na namna ya kuyaepuka.

Nao viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ambao ni Joasi Mganyizi Mwenyekiti wa chama naye mwenezi Yazidi Isacka nao wameungana na Madiwani katika kuupongeza mpango huo huku wakiilekeza Takukuru kuuhamasisha zaidi katika idara mbalimbali za kutolea huduma kwa umma kwakuanzia Polisi, Afya na mahakama kwani huko mara kadhaa kumekuwa kukilalamikiwa mno na wananchi kuhusika pakubwa na masuala ya rushwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!