Home Kitaifa TAFU WANASIASA MUACHE KUFANYA UVUVI KAMA AJENDA YA KISIASA.

TAFU WANASIASA MUACHE KUFANYA UVUVI KAMA AJENDA YA KISIASA.

Chama cha Wavuvi Tanzania ( TAFU ) kimewaomba wanasiasa wote nchini kujiepusha kufanya suala la uvuvi kuwa suala la kisiasa kutokana na baadhi ya wanasiasa kuanza kutoa lugha ambazo zinaweza kuchochea kufanya uvuvi ambao unaweza kuleta madhara ndani ya ziwa Victoria ikewemo uvuvi haramu.

‘’Hatuwezi kuepuka siasa na maisha yetu lakini tunaofika kwenye masuala ya kitaalamu wanasiasa watimize wajibu wao kwa kushauri tu, sisi kama wavuvi atuwezi kukubali ziwa Victoria ligeuke kuwa ajenda za uchaguzi mkuu wa Serikali katika majukwaa ya kisiasa, Bakari Kadabi – Mwenyekiti ChAma cha wavuvi Tanzania, Tafu.

Mwenyekiti wa Chama cha wavuvi Tanzania ( TAFU ) Bakari Kadabi amewaomba wanasiasa nchini watusaidie kuelimisha baadhi ya wavuvi , maafisa uvuvi , watendaji wa vijiji, wenyeviti wa serikali na wengineo wote kuacha kujihusisha na uvuvi haramu, ili waache na watambue umuhimu wa kulinda raslimali za nchi kwa faida ya Watanzania wote.

“ Tunaiomba Serikali ihakikishe samaki analindwa kama wanavyolindwa wanyama pori katika hifadhi za taifa na inasikitisha kuona maliasili zote zinalindwa kwa kutumia nguvu kubwa sana kuliko maliasili ya uvuvi, Bakari Kadabi – Mwenyekiti ChAma cha wavuvi Tanzania, Tafu.

Chama cha wavuvi Tanzania kikiongozwa na mwenyekiti wake Bakari Kadabi wamekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia suala zima la kulinda rasilmali ya samaki ndani ya ziwa Victoria kutokana na uwepo wa kushamiri kwa vitendo vya uvuvi haramu katika ziwa hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!