Home Kitaifa TADB WANUFAISHA VIJANA WAFUGAJI NCHINI WANUFAIKE KIUCHUMI

TADB WANUFAISHA VIJANA WAFUGAJI NCHINI WANUFAIKE KIUCHUMI

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kuwakwamua wafugaji kiuchumi ambapo wametoa mikopo katika sekta ya ufugaji shilingi bilioni 25 zimetolewa katika mnyololo wa thamani wa Mifugo hasa katika unenepeshaji wa Mifugo na ng’ombe wa maziwa.

Akitoa taarifa katika ufunguzi wa Maonyesho Jumuhia ya Wafugaji kibiashara nchini TCCS Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya TADB Frank Nyabundege huko Ubena Chalinze mkoani Pwani ambapo Wafugaji kiboashara na Wadau wake wanaonyesha shughuli zao.

Amesema kwa kuanzia mradi wa kuwezesha vijana ikiwa ni kuunga mkono Nia ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetaka kuona vijana Wafugaji wanawezeshwa bank hiyo imetenga shilingi milioni 279 kwaajili ya kukopesha vikundi vya vijana.

Amesema Bank hiyo huwasaidia vikundi vya vijana vyenye idadi ya vijana kuanza na vijana watano katika sekta ndogo ya maziwa na tumeanza katika mkoa wa Tanga kwakushirikiana na shirika la linaitwa solitalidad.

“Dhamira yetu ni kulenga vijana kujikwamua kiuchumi yaani kujiajili kupitia mradi huo ambapo vijana wanapewa mkopo kwa riba ya asilimia saba n walie kwa miaka saba ambapo pia mkopo huu unakwenda kumuwezesha kijana kununua shamba lenye ukubwa wa ekari tano mpaka kumi”

Amefafanua kuwa pia mikopo hiyo huwasaidia vijana kujenga nyumba ya kuishi na kujenga banda bora kwa ajili ya wa hao ng’ombe kufugia ng’ombe kumi na hao ng’ombe kumi wa maziwa, umwagiliaji katika shamba hilo la malisho na pia kupata vifaa kwa ajili ya kushiriki katika ufugaji.

Aidha Mkurugenzi huyo ameahidi kuendelea kufadhiri Maonyesho hayo ya wafugaji kiboashara kwa kusema “Sisi tutakuwa ndio wafadhiri wenu wakubwa kwa kadri mtakavyofanya maonyesho maana Rais wa Tanzania anawajali wananchi wake wote hasa wakulima na wafugaji, mwaka unaofata pia tutakuwa ndio wafadhili wa event hii”

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafugaji wa Kisasa Tanzania NCCS, Naweed Mulla amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan kutikana na serikali kuwashika mkono wafugaji wa kisasa.

Mulla amesema kuwa maonesho haya yanalenga kuwanyanyua wananchi na wafugaji wa kisasa pamoja na kuwawekea mazingira sahihi huku amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inasema tufuge kibiashara tuijenge kesho iliyo bora.

“Mhe.Rais amekua akitupa maneno ya kututia moyo pindi awapo katika majukwaa mbalimbali jambo ambalo linazidi kutuje nga na kutukuza zaidi” amesema Naweed.

Mwenyekiti huyo wa NCCS Naweed amesema kuwa Mh.Rais amewapa bajeti mara mbili kwa kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi hivyo tunaahidi kutoa ushirikiano wa kutoa maoni yetu katika sekta hii ya ufugaji wa kisasa na tuna ahidi tutakuwa naye begakwabega katika kukuza uchumi wa nchi kupitia ufugaji wa kisasa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti akifungua Maonyesho hayo aliwapongeza Jumuhia ya Wafugaji kibiashara kwa kufanya Maonyesho hayo yanayoonyesha Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara ambao utasaidia kuongea Soko la nyama ya Tanzania Kimataifa.

Tanzania ni nchi ya pili kwa mifugo barani Afrika pia tuna ng’ombe zaidi ya Mil.37.

Maonesho hayo yamefunguliwa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti yafungwa kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!