Home Biashara TABWA YAWAFIKISHA CHINA WAFANYABIASHA WA TANZANIA

TABWA YAWAFIKISHA CHINA WAFANYABIASHA WA TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiasha wanawake Tanzania (TABWA), Bi.Noreen Mawalla (katikati), akiongoza jopo la Wafanyabiasha zaidi ya 50 Kutoka Tanzania,  walipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Pudong Jijini Shanghai katika ziara ya kibiashara. nchini China.

Wafanyabiasha hao watatembelea Mji wa Shanghai na Yiwu wenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali za viwandani, na kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Canton Fair yanayorajiwa kuanza rasmi tarehe 15, hadi 25, 2023 katika Jiji la Guangzhou nchini humo, chini ya uratibu wa Taasisi ya TABWA kupitia ufadhili wa Kampuni ya  Professional Exchange Platform ((Pexpla).

Wafanyabiasha hao wamesafiri na Shirika la ndege la Emirates kupitia Dubai na baadae kuendelea na safari yao kwa ndege ya Shirika hilo hadi nchini China.

Wafanyabiasha Kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Pudong Jijini Shanghai, China.

(PICHA NA: Hughes Dugilo, CHINA)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!