Home Kitaifa TAASISI YA TMFD YAINGIA MAKUBALIANO NA FUO KUENDELEZA SEKTA YA UVUVI NCHINI

TAASISI YA TMFD YAINGIA MAKUBALIANO NA FUO KUENDELEZA SEKTA YA UVUVI NCHINI

Na. Mwandishi wetu, Mwanza.

Taasisi ya Waandishi wa Habari wa kuendeleza shughuli za bahari na uvuvi Tanzania (TMFD) leo Juni 12, 2023 imeingia kwenye makubaliano na Chama cha umoja wa Wavuvi Tanzania (FUO) ya kufanya kazi kwa pamoja.

TMFD na FUO wamekubaliana kufanya kazi kwenye maeneo ya haki za binadamu, afya , ulinzi wa kijamii na tafiti.

Bwana Alphonce Tony Afisa Habari wa TMFD amesema kuwa, ushirikiano huo unalega kuimarisha shughuli za uchechemuzi kwa mashirika yote mawili na kusaidia uvuvi endelevu Nchini.

Naye Mkurugenzi wa FUO Bwana Juvenary Edmund Mtagili alisema kuwa wana furaha kufanya kazi na taasisi ya waandishi wa habari ya TMFD hivyo itasaidia shughuli zao kusikika kupitia vyombo vya habari.

TMFD inafanya kazi ya kuendeleza ahughuli za bahari na uvuvi Tanzania na kwa sasa ina mtadao wa redio za kijamii kwenye maeneo Ziwa na Bahari Tanzania

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!