Taasisi ya Saratani ya Babuu(BCF) ya Jijini Dar es salaam imeandaa Kampeni ya Saratani kitaa inayolenga kutoa elimu ya saratani kwa Jamii ya Mkoa wa mwanza pamoja na maeneo Jirani.
Mandingo amesema kuwa, kampeni hiyo itakayofanyika kesho Desemba 28 mwaka huu kwenye uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini Mwanza ambayo itatanguliwa na matembezi ya furaha ya umbali wa kilometa tano.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Jijini Mwanza,Mwenyekiti wa Taasisi ya BCF, Cedou Mandingo ‘BABUU WA KITAA amesema, kuwa matembezi hayo yatawaleta pamoja wananchi ili kuunga mkono mapambano ya saratani, kupata elimu, kukutana na wataalamu na watoa huduma za afya sanjari na kuzifikia familia za wagonjwa wa saratani.
Kwa upande wake, Daktari bingwa wa saratani Dokta Frank rutachunzibwa amesema kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa saratani nchini wanatokea mikoa ya kanda ya ziwa ambapo tafiti zinaendelea kufanyika ili kubaini sababu zinazochangia kuwepo kwa tatizo hilo.
Amesema kuwa elimu itakayotolewa wakati wa kampeni hiyo inalenga pia kuhamasisha jamii kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara na kupatiwa matibabu wale wanaobainika kuwa na ugonjwa wa saratani ikiwa kwenye hatua za awali.