Home Afya TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAWAFIKIA WANANCHI KAGERA UCHUNGUZI WA SARATANI

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAWAFIKIA WANANCHI KAGERA UCHUNGUZI WA SARATANI

Na Theophilida Felician Kagera.

Taasisi ya Saratani Ocean Raod ipo Mkoani Kagera kuanzia leo Tarahe 31 Oktoba mpaka Tarehe 2 mwaka huu wa 2023 ikiendelea na utoaji huduma ya uchunguzi wa Saratani kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na meneja wa huduma ya kinga ya Saratani katika Taasisi hiyo Dr Maguha Stephano wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba.

Maguha amesema kuwa wamefika Mkoani Kagera kutoa huduma ya uchunguzi wa Saratani kwa wananchi kwa malengo ya wakuwasogezea huduma hiyo karibu kwani huduma hizo kwakiwango kikubwa ziko mbali na maeneo yawananchi hapa nchini hivyo kwakuwafikia karibu kupitia Hospitari za rufaa itakuwa vyema wananchi kujitokeza nakupata huduma hiyo kwa ukaribu.

Amebainisha kwamba wamefika Kagera kuendesha kampeni hiyo ili kuwasaidia wananchi huduma mbalimbali ikiwemo hiyo ya uchunguzi sambamba na kutoa elimu juu ya ugonjwa huo kwa umma.

“Sisi kama Taasis ya Ocean Road tumeona ni vyema kufika katika Hospitali za rufaa za mikoa hususani maeneo ambayo ni mbali na Dar es salaam ambako Taasisi ipo ya huduma hizi za Saratani, pia niagizo la Mhe Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassani kwamba Hospitali za kibingwa ziwe zinakuja katika Hospitali za rufaa za mikoa ili kuweza kuwasaidia wananchi hasa hasa wale wakipato cha chini ambao hawawezi kuzifikia Hospitali za kibingwa kupata huduma hizi, kwahiyo tuko hapa siku hizo tatu kwa ajili ya kueleimisha umma na kufanya uchunguzi wa Saratani hizo” ameleeza Meneja Maguha Stephano.

Amefafanua kuwa ugonjwa wa Saratani umekuwa ukiongezeka kutokana na sababu mbalimbali ambapo kwa takwimu za mwaka jana 2022 kwa upande wa akina mama Saratani ambayo iliongoza kuwa na wagonjwa wengi ni Saratani ya mlango wa kizazi ikifuatiwa na Saratani ya matiti huku saratani ya koo la chakula ikiongoza kwa upande wa wanaume ikifuatiwa na saratani ya tezi dume.

Meneja huyo amesema kuwa huduma hizo za uchunguzi kwa Saratani za titi, mlango wa kizazi, koo la chakula na tezi dume zinatolewa bila ya malipo.

“Uchunguzi huu tunafanya bila malipo kwahiyo nawale wote ambao wataonekana na viashiria vya awali vya Saratani hususani Saratani ya mlango wa uzazi timu ya madakitari bingwa kutoka Taasisi ya Ocean Road na madakitari wengine tuko hapa kwa ajili ya kutoa matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani lakini pia kwa wale watakaoonekana wana dalili za Saratani tutatoa vipimo vya vinyama na kuvifanyia uchunguzi ambao watabainika kuwa na saratani tutawapa rufaa kwenda Taasisi ya Ocean Raod kutibiwa ama Bugando” ameendelea kutoa ufafanuzi kwa undani meneja huyo Maguha Stephano.

Hata hivyo ameongeza kuwa ugonjwa wa Saratani siyo wakuambukiza isipokuwa tuu unatokana na mabadiliko ya chembe chembe hai ambazo ziko kwenye miili ya binadamu.

Amezitaja dalili ya Saratani kulingana na utofauti wake ikiwemo ya kuwa na uvimbe unaotokea sehemu husika ya mwili Saratani ilipo ambapo ametole mfano wa Saratani ya titi inakuwa na dalili ya uvimbe sehemu ya titi, kwa pani, chuchu kubonyea ndani au kutoa damu na maji maji meusi na nyinginezo.

Kwa upande wa Saratani ya mlango wa uzazi amesema kunakuwa na uvimbe kwenye mlango wa uzazi pamoja na kutokwa damu ukeni sisizo zakawaida yaani hata kwa mwanamke aliyekwisha koma hedhi.

Pia amehimiza wanaume kujitokeza kwa wingi ili nao waweze kufanya uchunguzi na vipimo vya Saratani ya titi na tezi dume kwani vipimo hivyo vya tezi dume ni vyakawaida hupimwa kupitia damu na kwa muda mfupi.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza nakuweza kunufaika na huduma hiyo kwani itawasaidia zaidi maana Saratani ikigundulika mapema inatibika.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma hiyo akiwemo Jaysce Mgayuki na Sara Kamugisha wameelezea kufurahishwa na ujio wa huduma hiyo Mkoani Kagera kwani itawasaidia vyema katika kutambua hali ya afya zao dhidi ya Saratani nakuwawezesha kupata matibabu kwa wale watakaokuwa wamebainika kuwa na dalili za ugonjwa huo hivyo wamewasihi wananchi wengine kujitokeza kwa kasi nakuwahi huduma hiyo muhimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!