Home Kitaifa TAASISI YA MWALIMU NYERERE YAWAKUMBUSHA VIJANA KILIMO CHA MANUFAA

TAASISI YA MWALIMU NYERERE YAWAKUMBUSHA VIJANA KILIMO CHA MANUFAA

Na Shomari Binda-Musoma

TAASISI ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imewakumbusha vijana kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo ili kuweza kupata manufaa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa mkoa wa Mara wa taasisi hiyo Emmanuel Masse alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la vijana wa Tanzania Youth Agro Irrigation Development Nertwerk Programme mjini Musoma.

Amesema lengo la kuanzishwa kwa kwa taasisi hiyo ni pamoja na kuwakumbusha vijana masuala mbalimbali yakiwemo ya kilimo ambayo kwa sasa serikali ya awamu ya 6 imeipa kipaumbele.

Akizungumza na vijana hao zaidi ya 300 wsnaojishughulisha na kilimo kwenye ukumbi wa mikutano wa uwekezaji uliopo ofisi ya mkoa wa Mara amesema watapata manufaa iwapo watawadikiliza wataalamu.

Amesema ili kupata mazao bora shambani na kuyapeleka sokoni utaalamu wa kilimo bora unahitajika na hiyo kazi hufanywa na wataalamu.

Masse amewaasa vijana hao kuwasikiliza wataalamu pale wanapokuwa wanawatembelea kwenye mashamba yao na kuwaelekeza namna ya kufanya.

Amesema uzalendo unawaokumbushwa na na taasisi ya Mwalimu Nyerere una dhamira njema hasa katika masuala yanayohusu vijana.

“Nashukuru kualikwa kwenye kongamano hili la vijana mnaojishughulisha na kilimo nami wito wangu no kuwakumbusha kuwasikiliza wataalamu wa kilimo wanapokuwa wanawatembelea” ,amesema Masse.

Amesema hivi karibuni kuelekea maadhimisho ya miaka 23 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere watafanya makongamano ya kuwakumbusha vijana masuala mbalimbali ya falsafa zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!