Home Kitaifa TAASISI YA MAZINGIRA NCHINI INDIA KUJIFUNZA MFUMO WA TAKA SIFURI MTAA WA...

TAASISI YA MAZINGIRA NCHINI INDIA KUJIFUNZA MFUMO WA TAKA SIFURI MTAA WA BONYOKWA

Na Magreth Mbinga

Taasisi ya mazingira kutoka Nchini India leo Julai 14 wametembelea kituo cha mfumo wa taka sifuri kilichopo Mtaa wa Bonyokwa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam ambacho kina chakata taka na kuwezesha kutumika kwa matumizi mengine kuona jinsi kituo hiko kinavyofanya kazi ya kusaidia kutunza mazingira ya Mtaa huo.

Hayo yamezungumzwa na Afisa Afya Mwandamizi wa Jiji la Dar es Salaam na Kata ya Vingunguti Ndugu Geofrey Zanda na kusema kuwa kulikuwa na work shop ya siku mbili pamoja na kufanya utafiti wa utunzaji wa mazingira.

Aidha Zanda amesema taasisi hiyo imekuja kujifunza na kuchukua taarifa za tafiti ambazo wanafanya sambamba na kuwawezesha kuwatengenezea dampo kila sehemu kwaajili ya kutupa taka ambazo hazina matumizi tena zisizagae mitaani.

Wanataka kuhakikisha usafi mwambao wa bahari unaimarika ili kutunza mazingira hayo ambayo yanaathiriwa sana na taka ambazo zinaweza kuchakatwa kama chupa na nyinginezo “amesema Zanda.

Pia Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa na Barozi wa Mfumo wa Taka Sifuri Tanzania Ndugu Shabani Maliyatabu amesema mfumo huo umefika kwenye Serikali kuu na wageni kutoka Nje ya Nchi wanakuja kujifunza jinsi unavyofanya kazi.

Sanjari na hayo Maliyatabu amesema wananchi wa Binyokwa ndio wamiliki wa mfumo huo wa taka sifuri pia kuna mabalozi ambao wanasimamia na kusaidia kutoa elimu wakipewa nguvu na Serikali ya Mtaa sambamba na taasisi ya Nipe fagio imewapatia vifaa vya usafi.

Bonyokwa ni sehemu ya utalii kwa sasa nawakaribisha Viongozi wote kuanzia Mawaziri, Wabunge, Madiwani ,Wenyeviti wa Mitaa bila kuwasahau Wananchi wa maeneo mbalimbali kuja kujionea na kujifunza njia sahihi ya kutunza mazingira na kutengeneza bidhaa kutimia taka” amesema Maliyatabu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!