Home Kitaifa TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MKOA WA PWANI YASAIDIA WATOTO NJITI

TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MKOA WA PWANI YASAIDIA WATOTO NJITI

Na Scolastica Msewa, Kibaha

Tasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Pwani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameadhimisha kilele cha siku ya watoto njiti kwa kutoa misaada ya mahitaji muhimu inayolenga kusaidia kundi hilo kwenye nyanja za elimu na afya kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila wakati wa kuadhimisha siku ya (Watoto Njiti) Duniani.

Misaada hiyo ambayo ni saruji, sabuni, mafuta ya watoto na mavazi ya michezo vimetolewa kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Hospital ya Mloganzira,Shule ya Msingi Kambarage na Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Pwani Omary Punzi amesema kuwa wamefikia hatua hiyo ili kuendelea kutimiza malengo ya taasisi hiyo ambayo ni mapambano dhidi ya ujinga ,maradhi na uamsikini.

Amesema kuwa mbali na hilo pia hatua hiyo inalenga kuikumbusha jamii ili kutambua kuwa bado tatizo la watoto njiti lipo na linaendelea kuwaandama wajawazito wengi hivyo ni vema ikapewa kipaumbele na kuongeza nguvu katika kukabiliana nalo.

Hili tatizo lipo na linaendelea kuisumbua jamii lakini limeanza kusahauika na likisahaurika litapungua nguvu ya kutafuta ufumbuzi kwa walengwa”amesema

Amesema kuwa Taasisi hiyo imeendelea kutekeleza malengo yake kwa kujiweka karibu na jamii ambapo katika msaada huo imeshirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wakala wa huduma za misitu kanda ya mashariki (TFS) ambao pia wanathamini wananchi.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi kambarage happynes tesha amesema kuwa msaaada wa mifuko 50 ya saruji iliyotolewa na taasisi hiyo itaongeza nguvu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea shuleni hapo

Naye kaimu mkuu wa shule ya msingi mtambani Sikitu Dibwe amesema kuwa msaada wa nguo za michezo walizopata kutoka kwenye Taasisi hiyo utasaidia wanafunzi kucheza michezo ambayo ni sehemu ya kuchangamsha akili.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi huduma za tiba wa Hospital ya mloganzira Dk Faraja Chiwanga amesema kuwa ,kati ya wajawazito milioni 2 wanaojifungua nchini laki 2 wanajifungua watoto kabla ya wakati( (njiti) huku sababu mbalimbali zikitajwa kuchangia hali hiyo ambazo ni pamoja na magonjwa yasiyoambukizwa na hata ukosefu wa lishe bora.

Amezitaja sababu zinazosababisha baadhi ya wajawazito kujifungua watoto kabla ya wakati(njiti) kuwa ni pamoja na kukabiliwa na maggonjwa yasiyo ya kuambukizwa pamoja na ukosefu wa lishe bora huku akitoa wito kwa jamii kuzingatia ushauri kutoka kwa watlaalamu wa afya ili kuepuka changamoto hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!