Home Biashara HAJI MANARA AZIDI KUWAKA NJE YA MPIRA APATA DILI NENE BAYPORT

HAJI MANARA AZIDI KUWAKA NJE YA MPIRA APATA DILI NENE BAYPORT

Na Magreth Mbinga

Aliyekuwa Msemaji wa Young Africans Haji Manara amesema amewataka wachezaji wenye majina makubwa kitumia majina yao na mitandao ya kijamii kijiongezea kipato nje ya mpira .

Amezungumza hayo leo wakati wa kusaini mkataba na taasisi ya fedha ya BAYPORT ambayo inatoa mkopo kidijitali kwa watumishi wa Umma na kusema kuwa yeye hana jambo dogo .

“Nikiliingia jambo nalifanya kwa ukubwa uleule nawaahidi nitafanya kazi wanipe uahirikiano katika kipindi chote cha mkataba lakini pia naahidi kwamba ujumbe ambao mnataka ufike utafika na utafika vile ambavyo matarajio yenu” amesema Haji Manara.

Aidha amesema BAYPORT ipo kwa mujibu wa sheria za nchi lakini inafata misingi ya kanuni za benki kuu ya Nchi yaani wanapotoa mikopo kwa watumishi wa Umma ili afanye kazi na taasisi ya kifedha lazima ajiridhishe kuwa inamanufaa kwa Umma.

“Taasisi hii ni kubwa na ipo kwa mujibu wa sheria mtumishi wa Umma ina miaka 16 katika utoaji huduma ya fedha na inatoa mkopo ndani ya saa 24 “amesema Haji Manara.

Pia uendeshaji wa BAYPORT Ndugu Nderingo Materu amesema BAYPORT ndani ya miaka 16 kuna vitu wamejifunza mambo makuu mawili ambayo ni umuhimu wa muda na umuhimu wa gharama kwenye maisha.

“Sisi BAYPORT ni waasisi wa huduma ya kutoa mikopo kidigitali ikiwa na maana kwamba mtumishi wa Umma anapotaka mkopo anauwezo wa kupiga aimu tu na akapata mkopo papohapo hatumi karatasi yeyote wala kiambata chochote sauti yake na muhudumu wetu unapata mkopo “amesema Materu.

Sanjari na hayo Materu amesema jbo hilo la kihistoria wameona liende kihistoria ambapo mtumishi wa Umma leo anakaa nyumbani kwake akapata mkopo wake hayo yote wanafanya ili kurahisisha na kuokoa muda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!