Home Kitaifa TAARIFA KUHUSIANA NA MADAI YA WANANCHI 135 WALIOHAMIA MSOMERA

TAARIFA KUHUSIANA NA MADAI YA WANANCHI 135 WALIOHAMIA MSOMERA

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imetoa ufafanuzi kwa umma kuhusiana na madai ya wananchi 135 waliohamia katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga wakitokea ndani ya hifadhi ya Ngorongoro yaliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari wakidai kutotendewa haki katika mchakato wa zoezi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Meneja Uhusiano kwa Umma Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Hamis Dambaya Aprili 10, 2024 imeeleza kuwa Mamlaka ilipokea barua hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni tarehe 03.05.2023 na kuifanyia kazi na majibu kuwasilishwa kwa wahusika tarehe 20.07.2023.

Imeeleza kuwa katika majibu hayo Mamlaka iligundua kuwa wananchi 132 wanaodai kutolipwa stahiki zao walikuwa ni sehemu ya kaya ambazo stahiki zao zote zililipwa kwa Mkuu wa Kaya.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa Majina matatu ambayo yameongezeka katika taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari, Mamlaka haijapokea malalamiko hayo kwa njia yoyote ile.

Hata hivyo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeeleza kuwa inaendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaotaka kuhama kwa hiyari kupata uelewa wa mkuu wa kaya ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa na msingi.

Pia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imetoa wito kwa baadhi ya vyombo vya habari kutafuta ukweli kwa kuwasiliana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro au Viongozi wa Serikali wenye mamlaka ya kusimamia zoezi la kuhama kwa hiari.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!